Hii ni baada ya msanii huyo kumpiga mtangazaji wa kituo cha radio cha Kiss FM Ezden chenye makao
yake jijini Mwanza, Ezden Jumanne aka The Rocker.
Akiongea kwa simu na Bongo 5, Ezden
amesema issue ilianza kabla ya ijumaa iliyopita ambapo alikuwa ameandaa show
iitwayo Mwanza Blast iliyoendana na uzinduzi wa mixtape ya rapper Nash MC
iitwayo ‘Mzimu wa Shaaban Robert’.
Amesema baada ya Dudubaya ambaye kwa
sasa yupo Mwanza kuona matangazo ya show hiyo alianza kuponda mtaani kuwa show
hiyo haina maana na ‘itakula za uso.’
Ezden amesema kitendo cha yeye
kutomjumuisha kwenye roaster ya waliopanda kwenye show hiyo kilimuuma.
Dudu Baya aliamua kumtafuta Dj John
wa Radio Free Africa kumuomba nafasi ya kupanda kwenye stage ya show hiyo kwa
malipo kiduchu lakini alikataa na kumwambia amtafute Ezden kwakuwa yeye ndio
mwamuzi wa kila kitu.
Msanii huyo aliyewahi kutamba na kibao cha Nakupenda tu, alimtafuta Ezden kibabe zaidi na alipompata akaanza kumporomoshea matusi ya nguoni kitendo kilichomfanya mtangazaji huyo kujibu.
Kuona hivyo Dudu Baya aliyekuwa
kwenye gari aina ya Noah alitoka nje kwa hasira na kumrushia kibao Ezden
kilichomparaza usoni.
Hata hivyo Ezden aliyekuwa
ameambatana na mtangazaji mwingine wa Passion FM, Filbert Kabago alisaidiwa na
mtangazaji mwenzake aliyemrushia ngumi Dudu kuinunua kesi.
Kutokana na picha hiyo,watu walijaa
katika eneo la tukio huku watu wanaomfahamu Ezden wakiomba ruhusa ya
kumfundisha adabu Dudu ambaye baada kuona nguvu ya umma inataka kumwangukia
alifyata mkia na kuondoka eneo hilo.
Baada ya muda kupita Dudubaya
alimtuma mtu kwa Ezden ili wayamalize kiume lakini Ezden amesema alipokutana
naye tena alijuta kufanya hivyo kutokana na msanii huyo mwenye sifa ya ubabe
kuleta michongo ile ile!
“Ujue mi nimemkaushia, coz alizingua
kinoma hadi kunirushia mkono mimi kisa nimemchana kuwa stage yetu hapandi…!
Nilitegemea angekua wa kwanza kusupport coz hizi ni harakat za muziki wa Mwanza
place anayotokea. Sasa hizi harakati za wapi za kutukana na kupigana na
waliokubeba? KUKATA RINGI KUBAYA. Ila poa.” Aliandika Ezden kwenye Facebook.
Ezden aliamua kuripoti polisi tukio
hilo japo show hiyo ilifanyika kama kawaida kwenye ukumbi wa Villa Park huku
Chege, Temba, Dark Master na wasanii wengine wa Mwanza walitumbuiza.
No comments:
Post a Comment