Joseph Lyimo,Mbulu
MADAKTARI
kumi wa Hospitali ya Haydom wilayani Mbulu katika Mkoa wa Manyara,
wameungana na madaktari wa hospitali za Serikali nchini, katika mgomo
wao unaondelea
Madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa inayotoa huduma zake kwa wagonjwa
kutoka katika Mikoa ya Manyara na Singida, walianza kugoma juzi.Hatua
hiyo imesababisha madaktari wengine wanaoendelea na kazi, kuelemewa na
wingi wa wagonjwa.
Hospitali hiyo ya Haydom, inamilikiwa na
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), lakini inapata vifaa
tiba na dawa kutoka serikalini.Wakizungumza na waandishi wa habari kwa
masharti ya kutotajwa majina, madaktari hao wanafanya masoma kwa vitendo
katika hospitali hiyo, walisema hawataendea kutoa huduma hadi madai yao
yatakapotimizwa.
Pia walilaani vikali tukio la kutekwa nyara na
kujeruhiwa vibaya kwa Dk Ulimboka ."Hata hivyo sisi tunaendeleza
mapambano ya kudai haki zetu kwa njia ya mgomo. Kwa nini wanatumia mbinu
chafu za kijasusi kushumghulikia Dk Ulimboka," alisema mmoja wa
madaktari hao.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Anatory Choya, hatua ya madaktari katika Hospitali ya Haydom, kuingia katika mgomo.
Alisema hata hivyo, ofisi yake inaendelea na jitihada za kuzungumza nao, ili warejee kazini na kuwahudumia wananchi.
Choya
alisema kwa sasa madaktari wanaoendelea na kazi ,wameelemewa na mzigo
wa kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa."Tulijaribu kuwaita ili tukae nao
katika meza moja, lakini walikataa. Hata hivyo tunamshukuru Mungu kwamba
tangu walipogoma hakuna madhara yaliyotokea kwa wagonjwa waliopo
hospitalini ," alisema Choya.
|
|
No comments:
Post a Comment