Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak bado hajapata fahamu na
anaendelea kusaidiwa kupumua kutumia mashine katika hospitali ya
kijeshi iliyoko kitongoji cha Maadi mjini Cairo.
Mubarak, mwenye umri wa miaka 84, yuko katika hali mahututi baada ya kupatwa na kiharusi hapo jana. Awali taarifa zilijitokeza kwamba kiongozi huyo wa zamani alikuwa amefariki dunia.
Wakili wake alisema jana hali ya Mubarak ilikuwa mbaya kutokana na ukosefu wa matibabu katika hospitali ya gereza lililo karibu na mji mkuu Cairo, ambako Mubarak amekuwa akitumikia kifungo cha maisha.

No comments:
Post a Comment