Na Yaqoub Nyembo
“Ukiona Nyoka anajinyoosha, ujue safari ndio imeanza tayar. “Tanzania kwa hili la Malawi mtajiumiza……………hamko sawa kwa sababu za mipaka labda kuna kingine”
Ndugu zangu, huenda mnafuatilia vizuri
tatizo la mpaka wetu wa Ziwa Nyasa na Malawi! Nilishtushwa sana na
hotuba ya Bwana Waziri. Mimi napenda utaifa wangu na uzalendo wangu.
Lakini napenda sana kutetea mambo yangu kwa kuukubali ukweli, kujua
facts zaidi, kukubali hata zile zinazonipinga na ndipo najipanga kujenga
hoja.
Sidhani kama nipo sahihi zaidi na lengo
langu si kusema nani anamiliki nini! Ukweli naoufahamu, tatizo si kubwa
kivile kama tunavyolifikiri kama tutachukua muda kupitia documents zote
na muhimu. Tunahitaji kwenda Public Records Office-Uingereza, Colonial
Archives Potsdam, Ujerumani, pia Malawi National Archives, Tanzania
National Archives, Libraries za UDSM na Chancellor College Malawi.
Naamini ubishi utaisha kwa kuwa documents zote zipo.
Angalizo:
Ziwa Nyasa liligawanywa na mabeberu wa kiingereza, kijerumani na kireno. Mkataba wa 1890 uitwao Anglo-German Agrrement unasema mpaka wa German East Africa(Tanzania bara ya leo) na Nyasaland (Malawi ya leo) unapita kandokando ya Ziwa Nyasa kutoka mto Ruvuma mpaka mto Songwe! Huu ni mkataba wenyewe, upo katika documents nyingi sana…..!! International Law inajua hili na International Lawyers wanaelewa nini nazungumza!

Sehemu nyingine ilikuwa ni 1891 kati ya
Ujerumani na Ureno. Mpaka ulianzia mto Ruvuma kuelekea Portuguese East
Africa(Msumbiji ya leo) na pia Ureno ikawekeana mpaka na British
Nyasaland (Malawi). Kwahiyo, kipindi cha Ujerumani, mpaka unasomeka ‘it
passes along the shore of the lake (Nyasa).
Mabadiliko ya mipaka:
Kipindi cha kikoloni, kabla ya Mjerumani kuondoka, marekebisho ya mipaka yalifanyika kati ya Mjerumani na Mreno kwa kusogeza mpaka mbele 0.5 KM from the original tripartite point. Na vijisiwa vya mto Ruvuma vikagawanywa. Mpaka leo ipo hivyo. Na eneo lingine ni kati ya Mwingereza na Mreno, ambapo kisiwa kilichopo eneo la Malawi linamilikiwa na Msumbiji mpaka leo na eneo la ardhi lililopo Msumbiji linakaliwa na Malawi. Huo ulikuwa mkataba wa marekebisho na ipo hivyo mpaka leo.

Kwahiyo, tulivyorithi mipaka, tumerithi
na mabadiliko haya na hivyo hatuwezi kugombana na Msumbiji wala Msumbiji
hawawezi kugombana na Malawi. Mpaka wetu na Malawi haukurekebishwa
popote pale mpaka mjerumani anatoka.
Marekebisho ya mipaka kipindi cha Uingereza:
Sote tunajua German East Africa, sisi pamoja na Ruanda na Burundi tuligawanywa katika sehemu mbili. Tukiwa chini ya League of Nations tukiangaliwa na Uingereza. Kuna mambo nahitaji tuweke sawa. tukaitwa Mandated Territory na Uingereza ni Mandatory power.

Turudi katika kamusi tutofautishe an
Annexed Colony and a Mandate! Mpaka ukawekwa kati ya Ubelgiji na
Uingereza. Nao uliitwa the MILNER-ORTS AGREEMENT OF 1922! Katika mkataba
huu, mto Kagera ulikatwa katikati na mpaka leo tumerithi hivyo.
Hapakuwa popote pale ambapo eneo la Ziwa Nyasa lilirekebishwa kwa njia
ya mkataba baina ya Nyasaland State na Tanganyika State, isipokuwa,
tofauti na Mandates zote, Tanganyika pekee, ilikuwa na tofauti ndogo,
ambapo, mpaka wa Ziwa Nyasa ukapewa kinachoitwa ‘wording’, na hivyo,
ramani ya Tanganyika na Official Records zikaonyesha kuwa mpaka umepita
katikati ya ziwa Nyasa!
Na hapa ndipo tatizo linapoanza na sisi
tumechukulia hii ndo Absolute Fact. Hatuendi mbele kidogo. Haya yapo
pale National Archives Secreatarita Files, Accession number AB 8 na AB
30! Nafikiri hotuba yote ya Waziri, ilitoka katika files hizi. Ndizo
walizopelekewa!!!
Twende mbele kidogo. Ni kweli, kama
mheshimiwa alivyosema, ramani nyingi kuanzia 1922 mpaka 1939 zinaonyesha
mpaka upo katikati ya ziwa! Je, ukweli huu utatutosha pekee mbeleni
tukifikishana mbali? Hapana! Mheshimiwa hakusema kuwa ramani zingine,
japo chache muda huu huu na Official Reports hazionyeshi mpaka au
zinaonyesha mpaka upo chini. Lakini ni chache! Kwanini hili? Bado
natafuta majibu
Lakini kwa haraka haraka, unaweza
ukasema kuwa Uingereza ilitamani Tanganyika iwe koloni lake na si
Mandate! Na pia ilishinikizwa na wawekezaji na hata jeshi ilisema
afadhali waiteke ili liwe koloni na waachane na Mandate! Nahitaji
tuelewe maana ya Mandate.
Hii yote ilitokea baada ya Donald
Cameroon, Governor wa Tanganyika kusema kuwa Tanganyika is a part of the
british empire and it will remain so! Hii ni siasa na si ukweli kama
unaelewa maana ya kuwa wao hawakuwa wamepewa koloni kama mali yao, bali
kuliangalia mapaka wananchi wapate ‘akili’ ili wapewe uhuru!
Kwa hiyo, kimsingi, kwa maana ya sheria
ya kimataifa, Tanganyika haikuwa sehemu ya British Empire kama yalivyo
makoloni yaliyotekwa mojakwa moja na Uingereza yenyewe! Hapa pakatokea
mvutano mkubwa sana katika House of Lords na House of Commons! Na hivyo
basi, mtafaruku huu wa mpaka ulianzia hapa, kwa kauli hii na hivyo hata
Waingereza wenyewe walivutana kuhusu mpaka.
Ipo hivi, mwaka 1926, wajumbe wa
mabaraza waliibana serikali iseme mipaka ya Tanganyika na ule wa Ziwa
Nyasa! Mabishano, kama haya yetu leo yalikuwa makubwa, ila si kwa
kutishiana kwa kuwa walikuwa wenyewe na walitaka kuwekana sawa! Ndipo
Secretary of State for Colonies alibanwa na mjadala ulikuwa wa kisheria
zaidi ukihoji status of the Mandate, British Empire, n.k; na kama
Waingereza wanamamlaka ya kujipangia kuhusu koloni waliolokabidhiwa
kuliangalia (nieleweke na si kulimiliki)! Mwishowe, mtu huyu mwenye
dhamana alisema kwamba, hata yeye anashindwa kuelewa, ‘what exactly is
the Sovereignty of Tanganyika lying’! Jamani mnamwelewa huyu mtu?
Kwa maana hiyo, haelwi vizuri mipaka
yetu, ambayo wenyewe ndo wameirekebisha au kuipa ‘wording’!! Hivyo,
tatizo linaanzia hapa na si muda mwingine wowote!!!
Kipi hakusema bwana mkubwa (Waziri wa Mambo ya Nje):
Kuanzia 1939, mambo yalibadilika na hawa hawa watu tunaochukua ushahidi kutoka kwao, wakafanya madudu! Na ilipoisha vita ya pili ya dunia, jamani oneni haya, hawa Waingereza katika ramani zao, tena nyingi mno,(kaangalieni East Africana Section, UDSM, sehemu ya thesis, kuna cabins 3 zimejaa ramani na bado ni mpya sana kutokana na kutunzwa na pia kutotumka sana), kumbe zinaonyesha bila shaka yoyote kuwa mpaka wa Tanganyika na Nyasaland unapita pembeni mwa ziwa na si katikati! mkuu hakusema hili. aliishia 1939!

Kumbe hawa jamaa walichora tena ramani
zote zikionyesha mpaka upo pembeni mwa ziwa!!!! Kwanini hili? Natafuta
majibu. Lakini kwa haraka naweza nika-speculate mawili;
Mosi, karibu na vita vya pili vya dunia,
ilisikika tetesi kule duniani kuwa, Ujerumani inarudi na inakuja
kuchukua malokoni yake. (kasome National archives of Tanzania,
Secreatariat files zote zenye kichwa cha habari, ‘the future of
Tanganyika in British Empire’). Kwa hiyo, Waingereza walihofia
kutimuliwa na kurudi kwa Wajerumani, na hivyo, wakarudisha ule mpaka wa
awali wa 1890! Pia, muda huu, baada ya kwisha vita, Tanganyika ikawa
chini ya UNO ambapo ilipewa Trusteeship Status!
Hii ni rahisi kuliko mandate.
Ilimaanisha to be granted immediate independence! Maana ya neno
immediate hapa ni kwamba, kwa tafsiri yangu, Waingereza walifahamu
wanatimka mapema mno kwani mkataba unasema hivyo….nafikiri, wakarudisha
ramani zikionyesha mpaka upo pembeni…na kitabu cha Nyasaland cha mwaka
1958, kinaonyesha mipaka ya Nyasaland na ziwa lote likiwa kwao!
Tukitaka kuwashinda Wamalawi, lazima
tukisome vizuri kipindi hiki na tuelewe facts zipi zinawapa kiburi na
zipi sisi tuzitumie, la sivyo, tunaweza………….!!!!!!!!!!!!! Kwahiyo future
of Tanganyika ilikuwa contested, uncertain, etc kipindi hiki, Pamoja na
mipaka yake pia!! Tujiulize, kwa maana ya mandate, Waingereza walikuwa
na Legal Authority ‘kurekebisha’ mpaka wa ziwa Nyasa? Na je makosa
waliyofanya Waingereza, ndo Legal backing yetu sisi? Ebu tuzame tena
tutafute facts tuwashinde hawa jamaa!
Tulishindwana na Uingereza kurekebisha
mipaka. Mwalimu alisubiri mpaka Malawi iwe huru! Akatoa miaka mitatu tu
na asingetambua mipaka ya kikoloni(soma hansard, 1962). Walipopata
uhuru, kukawa na matatizo ambayo Waziri wetu pia aliyaeleza. Nampongeza
ni dhahiri, 1964 Cabinet Crisis ya Malawi na wale mawaziri kutorokea
nchini kwetu kupitia ziwa, Banda akaona ziwa ni infiltration route!
Sera zetu za mambo ya nje zilikuwa
tofauti. Tulikuwa frontline state kwa ukombozi, wenzetu wakasapoti
makaburu na wareno na wakawa na balozi sehemu hizo…..wakagombana na
mwalimu, Military show down miaka ya 1967-8; matusi na kejeli zikatawala
kati ya Mwalimu na Banda, sisi na Malawi…..kipara cha Banda
kinamagamba, tuliimba tukiwa jeshini.
Mwalimu akasema mpaka a sensible leader
akitokea Malawi ndipo tutajadili tena swala hili na si na Kamuzu Banda!
Tulikuwa kimya. Na kuanzia 1975, hatukuwa na tatizo, lakini si kusema
kuwa tulitatua tatizo la mpaka! Tulikaa kimya!
Mipaka haina tatizo isipokuwa ni time
bomb ambapo ikitokea spark ni explosion! Tuliirithi kupitia Article III
ya OAU CHARTER ya 1964 BAADA YA DEBATES KUBWA NA WENGI WAKARIDHIA
TUIRITHI, uti possidetis, ita possidetis principle (so as you exist, so
may you exist), kama kawaida yetu tulidesa ya kibeberu, Westphalia
principle, border inviolabiliy! hatukupata muda mwingi wa kutafakari na
kuangalia kila mpaka na matatizo yake….tulirithi na matatizo na
yanatutatiza leo!!!
Way forward!
Naikiri tuna namna tatu ya kulimaliza!
Naikiri tuna namna tatu ya kulimaliza!
Moja ni kwa majadiliano ya kawaida yaani
diplomacy kama bwana mkubwa alivosema. Pili ni kupigana vita. (war is
another means of diplomacy), mnataka kuniona kichaa! Huo ndo ukweli,
atakayeshindwa atasalimu kama ilivyokuwa kwa Uganda na sisi. Tatu ni
mahakama ya kimataifa yaani International Court of Justice!
Hapa nina wasiwasi. Kama facts zenyewe
ni zile za jana tu, sijui kama tutatoka. Tutulie, tuite wataalamu wetu
wajikite ndani sana.
Ni kweli kama alivyosema bwana mkubwa
kwa kunukuu kesi nyingi na zilizoshinda, na kwa kusema kuwa, tukienda
mahakama ile sisi ndo tutashinda!!!ninashaka….tumejipa favour ya verdict
kabla ya kesi. Sijui. Ninashaka kubwa! Kunakushinda, kushindwa au
suluhu! Ninashaka tena na tena! mimi ni mzalendo. Nataka ukweli kwa njia
ya mahojiano na kuumiza kichwa. Tutetee mali zetu tukijua tunawashinda
kwa hoja…..!!!!
Wasiwasi:
Inasemekana kuna mafuta ziwani!!! Kwahiyo mjue Marekani na washirika wake hawako mbali! Tujue operation ya military imperialism na huyu mama, mpwa wa Kamuzu Banda, Anapata wapi hiki kiburi…nyuma yake kuna nini na nani!!1Tuangalie haya pia.

Hitimisho.
Tusiwe na hoja moja tu mkononi kama ndo water-tight evidence. Tujaribu kuzibishanisha hoja zetu. na hoja nzuri ni zile zinazopingana nasi na tusizozipenda, tukizielewa na kuzikubali ndipo tutajipanga namna ya kuzigalagaza. tumwelewe vizuri adui yetu…..
MUNGU IBARIKI TANZANIA!ZIWA NYASA!WANYASA!WATANZANIA!”

KUNA ZAIDI YA MIPAKA HIYO……!
No comments:
Post a Comment