Watengenezaji wa filamu dhidi ya Uislamu iliyozua wimbi la kimataifa
la maandamano watashtakiwa nchini Misri, Muendesha mashitaka
wa serikali ametangaza mashitaka dhidi ya watu saba kwa kuitusi
dini ya kiislamu na kuchochea machafuko ya kimadhehebu.
Mahakama haina mamlaka ya kuwalazimisha watengenezaji filamu hiyo kufika mbele ya mahakama hiyo, lakini kesi yao inaweza kusikilizwa bila wao kuwepo.
Tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo dhidi ya watu hao ambao wote wanatokea nchini Misri, haijapangwa. Mchungaji wa Kimarekani, Terry Jones, ambaye amesema anaiunga mkono filamu hiyo, pia atafunguliwa mashitaka.

No comments:
Post a Comment