Waasi wa Syria wamewaua wanajeshi 14 wa serikali kufuatia mashambulizi dhidi ya kituo cha kijeshi kwenye jimbo la Daraa hivi leo. Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binaadamu la Syria, mauaji hayo yamefanyika siku moja tu baada ya waasi hao kuwaua wanajeshi wengine 92.
Katika mji wa Aleppo, waasi hao pia wamefanikiwa kukiteka kituo cha kijeshi cha anga kilichopo mashariki mwa mji huo hivi leo. Mapigano yanaripotiwa kutokea katika kambi nyingine ya jeshi iliyo karibu na Maarat al-Nuaman, mji uliopo kwenye barabara kuu ya kaskazini mashariki mwa Aleppo.
Mji huo pia ulichukuliwa na waasi wiki hii. Wanaharakati wanaounga mkono upande a upinzani nchini humo, wamesema kuwa kiasi ya watu 260 wameuawa katika maeneo mbalimbali nchini Syria jana pekee.
Idadi ya wanajeshi wa serikali waliouawa tangu jana imepindukia 100, ikiwa ni hasara kubwa kabisa kwa serikali ndani ya siku chache tangu, kuanza kwa vuguvugu la upinzani dhidi ya utawala wa Rais Bashar al-Assad mwezi Machi mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment