Mazungumzo kati ya waasi wa M23 na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yaliyokuwa yakitarajiwa kuendelea leo mjini Kampala, yameahirishwa huku msemaji wa tawi la kisiasa la M23, Betra Bisimwa, akisema pande zote mbili zinapumzika.
Kilichoshuhudiwa hadi sasa kwenye vikao viwili vilivyopita ni pande zote kulaumiana mbele ya waandishi habari.
Waziri wa mambo ya kigeni wa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Raymond Tshibanda, alisema hapo jana wakati wa kuanza tena mazungumzo mjini Kampala kuwa waasi wa M23 wamefanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya raia na ukatili huo umeonekana na maafisa wa Umoja wa Mataifa.
Kundi la M23 ambalo liliundwa mapema mwaka huu kutokana na malalamiko katika jeshi la nchi hiyo, liliondoka kutoka mji wa Goma, mji ambao waliukamata kufuatia mashambulizi kadha dhidi ya jeshi la serikali na jeshi la umoja wa mataifa linalolinda amani katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment