Sheikh Hamad amesema kuwa mkutano unaofanyika mjini Marrakech, una umuhimu wa pekee, na kwamba unafanyika katika wakati ambao watu wa Syria wako karibu na kukamilisha ushindi wao na kufikia matakwa yao halali ambapo wamepoteza damu yao na roho zao. Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa Marekani kuutambua upinzani nchini Syria ni kukiuka makubaliano.
Wakati huo huo majeshi ya Syria yanasemekana kuwa yametumia mabomu ya kuteketeza katika maeneo wanakoishi watu wengi. Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch , limetoa wito kwa maafisa kuacha kutumia silaha ambazo zinasababisha hususan madhara makubwa ya kikatili kwa watu. Silaha hizo mara nyingi husababisha kuzuka kwa moto na kuchoma majengo ama kusababisha watu kuungua pamoja na matatizo ya kupumua.
No comments:
Post a Comment