Thursday, April 25, 2013

GARI LENYE VIFAA MAALUM VYA MAABARA LAZINDULIWA DAR KUTIBU KISUKARI NA PRESHA


Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii mheshimiwa  Dr Hussein  Ali Mwinyi amezindua rasmi gari lenye namba  T 466 CJR ,maalum kwa  huduma za upimaji wa afya kwa magonjwa yasioambukiza,hususan  kisukari na shinikizo la damu.

Uzinduzi huo umefanyika leo asubuhi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ,ambapo watu mbali mbali walipata fursa ya kipekee ya  kupima afya zao bure bila malipo magonjwa ya sukari na presha.

Waziri mwinyi amesema gari hilo litakuwa gari la kwanza Tanzania  litakalo kuwa lina vifaa maalum vya maabara,na  kwa kuanzia gari hilo litahudumu katika mikoa ya  kanda ya ziwa na hapo baadae litaenda mikoa mbali mbali nchi kutokana na ratiba itakavyopangwa.

Gari hilo limetolewa na msaada wa wold diabet  foundation ,chini ya mwanzilishi wake  Dr.kaushik Ramaiya,kwa chama cha cha kisukari Tanzania  ili kuhakikisha kuwa jamii ya watanzania wanapata huduma   ya magonjwa wa kisukari na presha kote nchini.

Aidha waziri mwinyi alieleza mkakati wa serikali ya Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa kisukari  kwa mpaka ifikapo mwaka 2017 kila kijiji kiwe na kituo cha afya .

waziri Mwinyi amewashukuru kampuni motorama inayosimamia magari aina ya Ashok leyland  nchini Tanzania(Watengenezaji wa gari hilo) kwa kuchagua gari hilo ambalo limefungwa vifaa vya kitaalamu na kwamba wamechagua gari ambalo linaendana na mazingira ya Tanzania .

Kwa kuhitimisha ufunguzi huo waziri wa afya  amesema anawashukuru world diabet kwa kutoa gari hilo na pia kuahidi kulihudumia kwa matengenezo yatakayohitajika kwa ushirikiano na mfuko wa wafanyakazi wa Novo nordisk ya nchini Dernmark.

No comments:

Post a Comment