Wednesday, April 24, 2013

NYUMBA NA OFISI ZA VIONGOZI ZACHOMWA MOTO HUKO LINDI


.
Hii ni nyumba ya Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia mwezi january 2013 wakati wa fujo za Mtwara ambazo pia zilisababisha kuchomwa kwa ofisi kadhaa za Serikali.
Mwandishi wa habari wa Radio One/ITV ambae pia ni mmiliki wa http://www.mchomeblog.com/  Reuben Mchome ameripoti kwamba nyumba mbili na ofisi mbili zimechomwa moto jioni ya April 23 2013 Liwale mkoani Lindi baada ya Wakulima wa korosho kushinda kuzuia hasira zao kutokana na kupunguziwa malipo ya mauzo ya mazao yao kutoka shilingi mia sita mpaka mia mbili kwa kilo moja.
Nyumba zilizochomwa moto ni pamoja na ya Mbunge wa Liwale Seif Mohamed Mitambo pamoja na ofisi yake ambapo nyumba nyingine iliyochomwa moto ni ya Mwenyekiti wa chama cha msingi Liwale B pamoja na ofisi yake vilevile.
.
Haya ni baadhi ya magari ya Halmashauri ya wilaya masasi yalipochomwa moto kwenye fujo za january 2013. (Picha zote zimepigwa na 
Happy Severine)
Mke wa Meneja wa chama cha msingi Ilulu amelazwa hospitali baada ya kupata mshtuko kutokana na nyumba kuvamiwa na kuchomwa moto ambapo jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati hizo vurugu kwa kupiga mabomu ya machozi kutawanya watu hao.

No comments:

Post a Comment