Tuesday, April 23, 2013

HIVI UNAJUA KUWA MSIBA WA KIDUDE ULISTUA ULIMWENGU

Field-Marshal ,Kamanda Ras Makunja(FFU),King of Anunnaki empire.jpg
Mahojiano Radio Zenj FM na Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band ! 

Kufuatia msiba wa mwanamuziki mkongwe barani afrika marehem Bi.Fatuma Bint Baraka (Bi.Kidude)
kama kawaida ya wanahabari walihakikisha wanasa wasanii na wanamuziki wa Tanzania hata kama wapo
mbali na Tanzania ili kusikia maoni na rambi rambi zao juu ya msiba huu.
Mtangazaji mashuhuri Bw.Mustapha Mussa wa Radio Zenj FM alimuhoji mwanamuziki Ebrahim Makunja
aka Kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi ya Ngoma Africa  yenye makao yake nchini Ujerumani.
Mwanamuziki huyo Ras Makunja alimtaja marehem Bi.Kidude kuwa sawa na jemedari,mwalimu wa walimu,
mpiganaji na balozi wa utamaduni wa waswahili na mwambao wa Afrika mashariki katika mataifa.
tafadhali endelea kusikiliza mahojiano hayo katika  audio

No comments:

Post a Comment