Jeshi la polisi nchini limefafanua juu ya
hatua mbalimbali zilizofikiwa juu ya kesi mbalimbali nchini na kusema kuwa
upelelezi wa kesi inayomkabili bwana
Wilfred Lwakatare pamoja na Ludovick Joseph umekamilika na jalada linaandaliwa
kwenda kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP)
kwa hatua zaidi.
Matukio ambayo ameyatolewa ufafanuzi ni
pamoja na matukio yaliyotokea Zanzibar,tukio la mhariri mtendaji wa habari
,bwana Absalom kibanda,Tukio la kumwagiwa tindikali
kada wa ccm bwana Musa Tesha katika uchaguzi mdogo na ubunge jimbo la
Igunga mkoani Tabora septemba 2011,tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dk.Ulimboka
,tuhuma za kuhusika na vitendo vya
kigaidi zinazomkabili mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na
maendeleo(CHADEMA) Bwana Wilfred Rwakatare na
Ludovick Joseph pamoja na matukio
mengine mengi yaliyoripotiwa katika
vituo mbali mbali vya polisi hapa
nchini.
Akieleza kuhusu kesi ya kwamwagiwa Tindikali
kada wa ccm bwana Mussa Tesha
katika uchaguzi mdogo wa Bunge jimbo la Igunga mkoani Tabora septemba 2011;watuhumiwa
wawili tayari wamefikishwa mahakamani na
upelelezi upo katika hatua za
mwisho,endapo watabainika watuhumiwa wengine nao watafikishwa mahakamani.
Kuhusiana na kesi ya kuvamiwa ,kupigwa
nakujeruhiwa mhariri wa New habari 2006 ,bwana Absalom Kibanda,tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dkt .Ulimboka 'matukio yaliyotokea huko
Zanzibar na matukio mengine yaliyoripotiwa katika vituo mbali mbali vya Polisi
hapa nchini,uchunguzi wa matukio haya
bado unaendelea na uko katika hatua mbali mbali za kupelelezi ambazo kwa sasa si
vema kuziweka wazi kuepusha kuharibu upelelezi unaoendelea.
Aidha kaimu mkurugenzi wa upepelezi wa
makosa ya jinai nchini DCP Issaya Mngulu amewashukuru wananchi
kwa ushirikiano wao mkubwa
unaosaidia kufanikisha upelelezi wa matukio ya uhalifu na hatimaye
kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu hapa nchini,pia amewaomba wananchi kuendelea
na ushirikiano huo ili nchi yetu iendelee kuwa salama.
Mwisho DCP
Issaya Mngulu ameomba kufahamisha umma wa watanzania kwa ujumla kwamba
zipo sheria na taratibu za kutoa habari na matukio yanayoripotiwa katika vituo
vya polisi ,ieleweke wazi kuwa taarifa zinaporipotiwa vituoni kwa mujibu wa
sheria ni za siri kwa faida ya wahanga
wa kesi na kwa ajili ya kufanikisha upelelezi wa kesi yenyewe ,aisha kanuni za
jeshi la Polisi zinaruhusu kamanda
kutoa taarifa za tukio na sio kujadili ushahidi wa kesi ili
kuepusha kuadhiri mwenendo mzima wa kesi ziwapo mahakamani.
Imetolewa na :
Issaya Mngulu DCP
kaimu mkurugenzi wa upelelezi makosa ya jinai
nchini.
No comments:
Post a Comment