Ndege maalum ya kivita itasindikiza Air Force One ya Rais Barack ObamaWalinzi wa rais Obama kama wanavyoonekana
MSAFARA wa Ndege ya Rais wa Marekani Barack Obama, yawezekana ndiyo msafara uliowai kupata ulinzi mkali kuliko zote.
Air Force One ambayo ndiyo ndege inayotumiwa na marais wote wa marekani,ndege hii ulindwa kwa asilimia mia moja.
Hata hivyo ulinzi wa ndege hii wakati wa utawala wa Rais Obama imekuwa tofauti baada ya kuongezewa ulinzi kuliko hata ilivyokuwa kwa mtangulizi wake George Bush.
Wakati wa Bush ndege hii ilikuwa inalindwa na ndege za kivita 10 lakini katika utawala wa Obama ndege hii inalindwa na ndege za kivita 15,wakati wote ikiwa angani.
AIR Force One hutembea katikati ya ndege sita za kijeshi,juu ya ndege ya Rais huwa kuna ndege mbili za kivita,chini ya ndege hiyo kuna ndege mbili, mbele ya ndege hiyo kuna ndege moja na nyuma kuna ndege moja.
Umbali wa kilomita 300 baada ya ndege ya Rais Obama kupita kuna kuwa na ndege mbili za kivita zenye mwendo kasi, kabla ya ndege ya Rais kupita kuna kuwa na ndege tisa zinazokwenda kwa mwendo kasi na sambamba kwa umbali wa kilomita zaidi ya 500.
No comments:
Post a Comment