Tuesday, June 25, 2013

WACHUNGAJI WAGUNDUA NJIA YA KUDUMISHA AMANI BAINA YA WAISALAMU NA WAKRISTO

MCHEZO WA MPIRA NI MCHEZO AMBAO UMEIBUKA KUWA MCHEZO UNAOPENDWA NA WATU MBALI MBALI MBALI WA RIKA TOFAUTI ,WA KIPATO CHA CHINI NA KIPATO CHA JUU PIA MPIRA UMEKUWA KIVUTIO KIKUBWA KWA WAUMINI WA MADHEHEBU MBALI MBALI HAPA NCHINI.

KATIKA MICHEZO YOTE ,MCHEZO AMBAO UNAWAKUTANISHA WATU MBALI MBALI HATA WAKATI MWINGINE  IMETOKEA KUWA KATIKA MBALI MBALI DUNIANI  KUNA MACHAFUKO MAKUBWA NA VITA INAKUWA IMEPAMBA MOTO HATA  KUSABABISHA  WATU  KUSHINDWA KUJITAFUTIA MAHITAJI YAO YA LAZIMA KAMA VYAKULA ,NGUO NA MALAZI.

IMEKUWA NI DESTURI KWA NCHI MBALI MBALI KUSIKIA NCHI FULANI IMENGIA KATIKA MACHAFUKO  MAKUBWA KISA TU  NI TOFAUTI ZA KIITIKADI ZA KIDIN AU WAKATI MWINGINE NI ITIKADI ZA KIDINI .


HAPA NCHINI KWETU  IKUMBUKWE KUWA KAMA SIO SERIKALI NA RAI WAKE KUWA MAKINI NA MSIMAMO PIA NCHI NAYO INGEKUWA KATIKA MACHAFUKO KUFUATIA  BAADHI YA VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI  ULIOTOKANA NA  UCHOCHEZI WA BAADHI YA WATU KWA KUTUMIA  VIVULI VYA DINI  ILI TU KUIPOTOSHA  JAMII NA KUHAKIKISHA KUWA AMANI YA WATU INATOWEKA.

IKUMBUKWE KUWA  KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM PIA KULISHATOKEA MACHAFUKO KAMA HAYO YALIYOHUSISHA WATU WALIJIWEKA CHINI YA MWAMVULI WA KIDINI ILI KUPOTOSHA JAMII NA KUPOTEZA AMANI AMBAPO  KANISA  LA KIINJILI LA KILUTHER  TANZANIA    HUKO MBAGALA LILICHOMWA MOTO NA KUHARIBIWA  VIBAYA KWA KANISA HILO NA MALI MBALI MBALI KUCHOMWA

KATIKA KUHAKIKISHA KUWA WANANCHI NA WAUMINI WA MAKANISA YA KIKIRSTO NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMI  WAMEUNGANISHWA KWA NJIA YA TIMU YA MPIRA  WA MIGUU AMBAO

NIKIONGEA NA  MCHUNGAJI KIONGOZI WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHER TANZANIA USHARIKA WA MBAGALA MCHUNGAJI  FRANK KIMAMBO   AMESEMA LENGO LA KUAMUA KUUNDA TIMU YENYE MCHANGANYIKO WA WAISALAMU NA WAKRISTO  NI KUHAKIKISHA KUWA WAISALAMU NA WAKIRSTO WANA KUWA  KITU KIMOJA NA   KUDUMISHA AMANI

TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA MBAGALA INA WAISLAMU 15 NA WAKRSTU 16 NA TIMU INAUNDWA NA WACHEZAJI 21 KUTOKA KATIKA  USHARIKA WA MABAGALA AMBAO KWA  USHIRIKIANO WAO WALIWEZA KUWAALIKWA WACHEZAJI WA  KUTOKA ZANZIBAR.

AKIONGEA NA GAZETI HILO MCHUNGAJI WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHER TANZANIA  HUKO ZANZIRA MCHANGAJI   LUSUNGU MBILINJI  AMESEMA KATIKA KANISA LAO HUKO ZANZIBAR LINAWAUNGANISHA  WAKRSTU NA WAISALAM KWA KUPITIA TIMU YA MPIRA YENYE WACHEZAJI 24 HUKU WAKIWA WAKRSTU NI 12 NA WANAISALMU NI 12 TIMU  YA ZANZIBAR INAITWA  YOUTH INTERFAITH  FORUM  YA ZANZIBAR

HAKIKA NI MFANO WA KUIGWA KWA MAKANISA HAYA MAWILI YA MBAGALA DAR ES SALAAM NA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHER  LA HUKO ZANZIBAR KWA KUAMUA KUWAUNGANISHA VIJANA  ILI KUDUMISHA AMANI KWA NJIA YA MPIRA WA MIGUU.

No comments:

Post a Comment