Tuesday, June 25, 2013

WENYE UJUZI KAZINI WASIO NA VYETI SASA KUPATA VYETI KUPITIA CHUO CHA VETA NA NAKTE

Veta ikishirkiana na  shirika la kazi duniani ILO imezindua  mfumo wa kutambua  ujuzi ulipatika kazini kwa wale wafanyakazi ambao hawajapitia vyuo vya mafunzo ya ufundi au kuhudhuria darasani ili kupata mafunzo kwa ajili ya taaluma au ujunzi wa mbali mbali .

Akiongea na  gazeti hili mkurugenzi wa mafunzo  wa veta bi Lea Doto Lukindo amesema veta ikishirikian na ILO imeamua kufufua  mafunzo ndani na nje ya kazi  katika nyanja mbali mbali za ajira  ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata nafasi ya kupata  vyeti vya kimataifa  vya veta au nekta ili kuweza  kuapata kazi kutokana na ujuzi ambao wameupata wakiwa kazni na kusema kuwa vyou vya Veta vinatoa nafasi kwa  wanavyuo kuweza kupata fursa ya  kusoma kwa muda mfupi  ili kuhakikisha kuwa wanapatiwa mafunzo mafupi  au ya muda mrefu ilia kuhakikisha kuwa wanakuwa na viwango hitajika na chuo cha Veta.


juhizi hizi za ILO na VETA kuanzisha  mfumo wa  kudahili wafanyakazi  kwa kutoa mafunzo  kwa wafanyakazi wakati wakiwa makazini , ni kuhakikisha kuwa  jamii na taifa kw ujumla inatambua  ujuzi ambao unapatikana kazini  ambao faida zake ni kama kupungua kwa ngarama za kujifunza kwani mfanyakazi atajifunza kwa kutumia vifaa sahihi na vilivyopo ofisini mwake , pia inasaidia kwa mwajiri kuweza k ujua nini anachohitaji hivyo kumkazia mfanyakazi kujifunza ili aweze kufanya kazi kwa usahihi.

Kwa kutumia mfumo huu wa k utoa mafunzo makazini  ,mwajiri anaweza kuandaa mtaala wa kufundishia  wafanyakazi wake ili waweze kufikia viwango stahili vya kampuni yake huku wakisimamiwa na vyuo vya veta au nakte kwa kuwa wao ndio wenye mamlaka ya kutoa vyeti  vya kitaifa ambao pia mwajiri ataifaidika na mafunzo haya kwani wakati mfanyakazi anapokuwa akiendelea kujifunza basi pia anakuwa anainua  uchumi wa nchi kwa kuwa atakuwa anaendelea na uzalishaji .

kwa upande wa viwango vya elimu ambavyo vitatolewa kwa mfumo huu  hakuna kitakachobadilika kwani Veta itatoa  maraja yale yale yanayotelewa na veta na pia nakte nayo itatoa vyeti kulingana na madaraja yake na pia itazingatia pia matokeo na uwezo wa mwanafunzi au mwajiriwa ambaye ameamua kufanya mafunzo ili aweze kupata vyeti vya kitaifa.

kubwa kabisa katika  mfumo huu ni utambuzi wa ujuzi binafsi au ujuzi ambao umepatikana kazini na njia ya kupata vyeti kwa kudhirhirisha uwezo wako kwa  kufanya mtihani kwa kile unachokijua  aidha kwa njia ya kufanya mtihani au kwa njia ya  kufanya mafunzo kwa vitendo .

mtaala huu utasaidia sana  kupunguza wanafaunzi ambao wanamaliza vyo mbali mbali na  kujikuta wakikosa kazi kwa kigezo cha kukosa  uwezo au uzoefu wa kufanya kazi .

No comments:

Post a Comment