Thursday, January 30, 2014

HUDUMA YA KUUNGANISHIWA UMEME YASHUSHWA KWA WANANCHI WA VIJIJI VINAVYOPITIWA NA BOMBA LA GESI MTWARA

Nanyumbu ,mtwara
Na mwandishi wetu Mercy Edgar.
 
 
Serikali imesema kuwa, bei ya kuunganisha umeme katika vijiji ambavyo bomba la kusafirisha gesi limepita , kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam,vijiji hivyo bei imeshushwa zaidi na kuwa shilingi 27,000 na itaanza kutumika mwaka huu.

Hayo yamesemwa na waziri wa nishati na madini profesa  Sospeter muhongo, wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme wilayani Nanyumbu, ambapo wilaya hiyo ndiyo wilaya pekee, ambayo makao yake makuu yalikuwa hayajaunganishwa na umeme.

Profesa Muhongo amesema kuwa wizara yake imefikia uamuzi huo, baada ya agizo la waziri mkuu ambaye aliitaka wizara ya nishati na madini, iangalie wananchi hao watakavyonufaika na bomba hilo ambalo linapita kwenye maeneo yao.

Muhongo amesema kuwa serikali inaendelea na juhudi za kupeleka umeme vijijini, ili ifikapo mwaka 2015, asilimia 30 ya watanzania wawe na huduma ya nishati hiyo, hivyo shirika la umeme Tanzania (Tanesco), limeagizwa kuwafungia wateja wapya wapatao 250,000 kutoka wateja 99,000 waliofungiwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment