Pichani
ni magari ya kuzolea taka ngumu ya kampuni mbalimbali yakiwa kwenye
foleni ya kuingia Dampo la Pugu Kinyamwezi ambalo miundo mbinu yake ni
mibovu na kupelekea zoezi hilo kuchukua zaidi ya siku 4 mpaka
kufanikisha kufikia eneo maalum la kumwagia taka ngumu.
.Ni kutokana na kukwama kwa magari ya taka kwenye Dampo la Pugu
.Siku ya tatu sasa magari ya taka yamekwama
Na. Mwandishi wetu,
MIUNDOMBINU
mibovu katika Dampo kuu la jiji la Dar es Salaam Pugu Kinyamwezi
imesababisha magari makubwa ya kuzoa na kumwaga taka kukwama kwa muda wa
siku tatu na kupunguza ufanisi wa kuzoa taka katika mkoa wa Dar es
Salaam.
Mtoa
taarifa wetu ambaye hakutaka kutajwa kwenye blogu hii, amesema kwamba
uongozi wa Dampo Pugu umeshidwa kuweka utaratibu mzuri na kukarabati
miundombinu ya dampo kwa muda mrefu na kusababisha msongamano mkubwa
wakati wa kwenda kumwaga taka katika sehemu hiyo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii jana asubuhi, mtoa taarifa (Jina
linahifadhiwa) amesema kwa muda wa wiki mbili sasa umwagaji wa taka
katika dampo hilo siyo mzuri kabisa na inaweza kufika miezi kadhaa tangu
dampo hilo lianze kuelemewa na uchafu kutoka kila kona ya jiji la Dar
es Salaam.
“hali
ni mbaya katika dampo la pugu kwa miezi kadhaa sasa na uongozi wa dampo
wameshidwa kufanya kazi kwa tija na kusababisha usumbufu mkubwa kwa
watumiaji wa dampo katika jiji la Dar es Salaam,’ amesema mtoa taarifa.
Amesema
magari makubwa aina ya (Bulldozers) hayawafanyi kazi kabisa na
kusababisha kukwama kwa kazi ya kumwaga taka katika dampo la Pugu
Kinyamwezi na msongamano mkubwa wa magari.
Mtoa
taarifa anasema kuwa kutokana na matatizo hayo katika dampo la Pugu
imesababisha baadhi ya taka kuoza kabisa na kuleta harufu kali kwa
wakazi wa karibu wa dampo hilo na tishio la magonjwa ya mlipuko ni
kubwa.
“kutokana
na tatizo hili katika dampo la hapa Pugu hali za kiafya kwa wakazi wa
karibu wa eneo ni ya hatari na magonjwa ya mlipuko yako mbioni kutokea,”
aliongeza.
Pichani
juu na chini hii ndio hali halisi ya muonekana wa eneo la Dampo la Pugu
Kinyamwezi. Kwa hali hii kweli jamani hata hayo magari ya kuzoa taka
yaliyopewa zabuni ya kukusanya taka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es
Salaam yatadumu kweli....???
Hivi
karibuni waandishi wa habari ikiwemo blog hii walitembelea eneo la
dampo na kufanya mahojiano na badhi ya madereva, Devera wa gari la
Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Ramadhani Sufi alisema adha
wanayoipata ni pamoja na kulala siku mbili na gari lenye mizigo ya taka
katika mazingira ambayo hawawezi kula kitu kwa hofu ya kupata magonjwa
ya mlipuko kama Kipindupindu.
‘tunawaomba
viongozi wa jiji kurekebisha hali hii ili waweze kutuepusha na magonjwa
hatarishi kutokana na uchafu unaorundikana mahali pamoja kuanzia kwenye
dampo hadi kwenye magari,” alisema.
Kwa
upande wake Dereva Rajab Kavuzi wa kampuni ya Tirima Enterprises,
amefafanua kuwa hali hiyo inasababisha kuwachafulia jina la kampuni yao
na kuonekana kama hawafanyi kazi kumbe tatizo lipo kwenye utaratibu
mzima wa Manispaa na suala la miundo mbinu.
Kwa
upande dereva mwingine Bw. Likongo wa Eco Protection alisema kero ya
kwenye dampo la taka lililopo maeneo ya Pugu Kinyamwezi ni za muda mrefu
ambapo taka zimerundikana hadi barabarani na njia hazipitiki hata
Magreda ya kuzoa hayana pakupita.
Gari la kampuni ya Tirima Enterprises likipita kwa shida kuelekea eneo maalum la kumwagia taka ngumu.
Ripota
wetu alifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Afya Mazingira wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam Bw. Membe Protus Membe ambaye
aliahidi kupambana na tatizo la mrundikano wa magari ya taka yaliyokwama
katika eneo la Dampo kutokana na ubovu wa miundo mbinu ya barabara
unaopelekea kukwamisha zoezi la ukusanyaji taka katika maeneo mbalimbali
ya jiji la Dar na kusababisha mrundikano wa taka nyingi kwa muda wa
siku tatu.
Lakini
mpaka sasa hali iko hivyo hivyo na imechukua takribani miezi sita tangu
atoe ahadi hiyo ya kutatua kero na ubovu wa miundombinu kuelekea dampo
la Pugu Kinyamwezi.
No comments:
Post a Comment