Baadhi ya pikipiki maarufu kama bodaboda zikiwa tayari kutolewa kwa washindi wa promosheni ya Timka na bodaboda inayoesndeshwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania mara baada ya droo iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo Bukoba mjini. Mpaka sasa jumla ya pikipiki 315 na jumla ya sh. 211 tayari zimetolewa hadi sasa, kushiriki na kushinda wateja wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
Meneja wa Vodacom Bukoba, Yusuph Mnga'gi akimkabidhi funguo Rashid Kagombora, mfanyabiashara wa Wilaya ya Muleba baada ya kushinda pikipiki katika shindano la Timka na Boda boda baada ya droo iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo Bukoba mjini. Mpaka sasa jumla ya pikipiki 315 na jumla ya sh. 211 tayari zimetolewa hadi sasa, kushiriki na kushinda wateja wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
Meneja wa Vodacom Bukoba, Yusuph Mnga'gi akimkabidhi funguo, Arnod Kaisi wakala wa forodha mpaka wa Mutukula Wilayani Missenyi baada ya kushinda pikipiki katika shindano la Timka na Boda boda baada ya droo iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo, Bukoba mjini. Mpaka sasa jumla ya pikipiki 315 na jumla ya sh. 211 tayari zimetolewa hadi sasa, kushiriki na kushinda wateja wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
*Wakazi wa Kagera wakabidhiwa Pikipiki zao.
*Mfanyabiashara wa Muleba na wakala wa forodha ni miongoni mwa washindi.
Na Mwandishi wetu, Kagera
ZIKIWA
zimebakia siku chache kabla ya kuisha kwa promosheni ya Timka na
bodaboda inayoendeshwa na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania
imeshuhudia wakazi wa Kagera wakikabidhiwa pikipiki zao zoezi
liliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo mkoani humo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi bodaboda hizo Meneja
wa Vodacom Bukoba, Yusuph Mnga'gi amesema kuwa wakati shindano hilo
likielekea ukingoni kampuni yao imeshuhudia mafanikio makubwa hasa
mikoani ambapo usafiri ni changamoto kubwa.
“Mpaka
sasa tumetoa jumla ya pikipiki 315 pamoja na sh. Milioni 211, Zawadi
hizi zimekuwa faraja ya kipekee kwa wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wengi
wanajishughulisha na shughuli za kilimo biashara ambazo zinahitaji
usafiri wa haraka ili kuongeza uzalishaji, ni imani yangu kuwa bodaboda
tunazozitoa leo zitakuwa msaada mkubwa kwao kwani sasa itawachukua muda
mfupi tu kusafirisha mazao yao kutoka shambani mpaka sokoni.” Alisema
Bw. Mang’agi
Meneja
Masoko huyo aliongezea kuwa kampuni yao imekuwa mstari wa mbele kwa kuwa
wabunifu wa huduma na bidhaa ambazo sio tu zitawanufaisha kimawasiliano
bali pia kuwainua kiuchumi na kufanya maisha kuwa nafuu.
“Kupitia
promosheni hii wateja wetu wameweza kujishindia usafiri wa bodaboda
ambao ni maarufu na kutumiwa na watu wengi nchi nzima. Pia wameweza
kujishindia fedha taslimu ambazo kwa kiasi kikubwa washindi wetu wametoa
ushuhuda kuwa watazitumia ipasavyo kama mitaji na kukuza biashara zao
ukizingatia wengi wamejiajiri katika shughuli zao bianafsi. Nawasihi
watu kuendelea kucheza zaidi kwani tunakaribia tamati nabado zawadi zipo
za kutosha tu.” Alimalizia Bw. Mang’agi
Naye
Bw. Rashid Kagombora, mfanyabiashara wa Muleba ambaye ni moja ya
washindi aliibuka kuwa mshindi wa bodaboda alibainisha kuwa usafiri wa
uhakika ni nguzo muhimu katika kuendeleza biashara na pia kujenga
uaminifu na mahusiano mazuri na wateja wangu pale unapowafikishia bidhaa
kwa wakati, hivyo naweza sema usafiri huu umekuja muda muafaka. Naamini
mwaka huu utakuwa wa mafanikio kwangu, nawashukuru kampuni ya Vodacom
kwa zawadi hii ya mwaka mpya kwangu waendelea kutujali kwa promosheni
hizi ambazo zinatunufaisha wateja wetu.
Mbali
na mfanyabiashara huyo, Bw. Arnold Kaisi, wakala wa forodha katika
mpaka wa Mutukula wilayani Missenyi alisema, “Sina la kusema kwa kweli
zaidi ya kuwashukuru Vodacom kwa pikipiki hii, nimekuwa nikipata tabu ya
usafiri kutoka nyumbani mpaka kazini ukizingatia siku zingine nachelewa
kurudi lakini kwa sasa nina usafiri binafsi hakuna shaka tena.” Alisema
Bw. Kaisi na kuongezea
“Kwa
ushindi huu nawaomba watu washiriki katika promosheni hii kwani
promosheni hii ni ya kweli na si longolongo, nimekuwa nikishiriki kwa
muda mrefu sasa na ningeshangaa kama shindano lingeisha bila ya kuibuka
mshindi.”
Wakati
promosheni hiyo ikielekea kuisha mapema mwishoni mwa mwezi huu, kampuni
ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imewataka wateja
wake kushiriki kwa wingi kwa kuandika neno PROMO kwenda nambari 15544.
No comments:
Post a Comment