Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye uzinduzi
wa mpango wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika halmshauri ya manispaa ya
Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae Resort mjini
Singida. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi.
Meneja
msaidizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Singida, Isaya
Shekifu, akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa
Singida.Dk.Parseko Kone, kuzindua mfuko wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika
manispaa ya Singida. Walioketi kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya
Iramba,Yahaya Nawanda na Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh
Salumu Mahami.
Mkuu
wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akitoa mada yake
iliyohusu mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwenye mkutano wa wadau wa afya
wa manispaa ya Singida.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(wa kwanza kulia) akisikiliza mada
zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano wa wadau wa afya wa manispaa ya
Singida. Wa kwanza kushoto,ni mstahiki meya wa manispaa ya
Singida,Sheikh Mahami.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha
ya pamoja na madiwani wa manispaa ya Singida.Walioketi wa kwanza kulia
ni Diwani wa viti maalum Yagi Kiaratu na anayefuatia ni mstahiki Meya wa
manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami.Kulia ni Katibu Tawala mkoa wa
Singida,Liana Hassan mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda na mkuu wa
wilaya ya Iramba na Queen Mlozi, mkuu wa wilaya ya Singida.(Picha na
Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WADAU
wa afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kauli moja
wameridhia kuanzishwa kwa Mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa
hiyo.
Wadau hao wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa mpango wa TIKA una
manufaa mengi ikiwemo mwananchi baada ya kulipa ada ya uanachama,
atakuwa na haki ya kupata huduma za matibabu ndani ya Manispaa kwa mwaka
mzima.
Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Mkoani Singida, Isaya Shekifu mpango wa TIKA ambao unafafana na Mfuko wa
Afya ya Jamii (CHF) unatumika mijini tu.
Shekifu amesema uanachama wa TIKA ni wa mtu mmoja mmoja, wakati ule wa CHF, ni wa familia au kikundi.
“Kwa sasa hapa Manispaa ya Singida, baada ya mpango huo kupata baraka
ya kuanzishwa tunaendelea na mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya CHF
kwenda kwenye Tiba kwa Kadi (TIKA)”,alifafanua Shekifu.
Meneja Msaidizi huyo amesema baada ya kukamilika kwa sheria ndogo
itakayotawala uendeshaji wa TIKA, mpango huo utaanza rasmi mapema
iwezekanavyo mwaka huu.
Akizindua mpango huo wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa ya Singida
juzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone amesema mpango wa TIKA
utawahakikisha wakazi wa Manispaa ya Singida na viunga vyake mwanzo
mpya wa kupata huduma za matibabu zenye uhakika.
Hata hivyo, Dk. Kone aliagiza viwango vya uchangiaji vya TIKA
zitazingatia uwezo wa mwananchi kulipia pia vitazingatia hali ya sasa ya
huduma za matibabu.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa kuwa suala la TIKA
ni la hiari wananchi watajiunga kwa wingi endapo watahamasishwa
kikamilifu.
“Kila mmoja hapa awe balozi mzuri kwa kuhamasisha wannachi wajiunge na
mpango huu mara baada ya sheria ndogo kupitishwa. Manispaa ihakikishe
huduma zinakuwa bora katika vituo vyote ikiwa ni pamoja na lugha nzuri
kwa wananchama”,amesema Dk.Kone.
No comments:
Post a Comment