Taliban wamekuwa wakiwaua wahudumu wa afya wanaotoa chanjo ya
Polio Pakistan
Watu waliojihami katika mji wa Karachi nchini Pakistan,
wamewaua kwa kuwapiga risasi wahudumu watatu wa afya wakiwemo wanawake wawili
waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio.
Hili ni shambulizi la hivi karibuni likiwalenga wahudumu wa afya wanaotoa
chanjo ya Polio au ugonjwa wa kupooza.
Walioshuhudia shambulio hilo walisema waliona watu waliokuwa wamejihami kwa
bunduki wakiwa wanaendesha Pikipiki wakiwapiga risasi wahudumu wa afya waliokuwa
wanatoa Chanjo hiyo kwa watoto wadogo.
Mwanamke mmoja alifariki papo hapo wakati mwingine alifariki akipelekwa
hospitalini.
Shambulizi hilo ni pigo kubwa kwa juhudi za Pakistan kupambana na ugonjwa huo
unaolemaza.
Kando na Afghanistan na Nigeria, Pakistan ni moja ya nchi ambako ugonjwa wa
Polio ni janga kubwa.
Wapiganaji wa Taliban wanapinga chanjo ya ugonjwa wa kupooza na wamekiri
kuwaua wafanyakazi wa afya wanaotoa chanjo hiyo nchini Pakistan.
No comments:
Post a Comment