Wednesday, January 22, 2014

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia apokelewa kwa shangwe alipowasili wizarani





Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Olegabriel akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam .

Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Bwana Clement Mshana (kushoto) akimpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia wakati wa mapokezi yake katika Ofisi za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam . Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Profesa Elisante Olegabriel.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bwana Kulwa Magingila wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam . Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fennela Mukangara akimkaribisha Naibu Waziri Mheshimiwa Juma Nkamia katika Ofisi za Wizara zilizopo katika jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF jijini Dar es Salaam .

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akiongea na Wanahabari Ofisini kwake katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam  kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Profesa Elisante Olegabriel.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiongea na Wanahabari, wakati wa mapokezi ya Naibu Waziri Mheshimiwa Juma Nkamia jijini Dar es Salaam . Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bwana Raphael Hokororo.

No comments:

Post a Comment