Wednesday, February 5, 2014

Taasisi ya Patel Brotherhood na Jumuiya za dini zakabidhi misaada ya sh. milioni 141 kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa ajili ya wananchi wa Morogoro, waliokumbwa na mafuriko

Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, akiwatambulisha baadhi ya wajumbe wa taasisi hiyo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, wakati walipofika Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam jana kwa ajili ya kukabidhi vifaa mbalimbali, vilivyotolewa na taasisi hiyo kwa pamoja na taasisi za dini kwa ajili ya wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko mkoani Morogoro. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuzungumza katika hafla hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk, Frolence Turuka na kulia ni Naibu wake, Regina Kikuli.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati alipofika kukabidhi vifaa mbalimbali, ikiwemo mabati, mashuka, biskuti pamoja na vitu vingine, vilivyotolewa kwa pamoja na taasisi hiyo na za dini kwa ajili ya wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko mkoani Morogoro, ofisini kwa Waziri Mkuu, Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati alipofika na viongozi wa taasisi nyingine za dini kwa ajili ya kukabidhi misaada kwa ajili ya wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza katika hafla hiyo, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel.
Baadhi ya wajumbe wa taasisi hizo, wakiwa katika hafla hiyo, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati alipokuwa akizungumza, Dar es Salaam jana.         
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa taasisi ya Patel Brotherhood na jumuiya za dini hizo, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, akiwa na baadhi ya viongozi wa dini na tasisi hiyo, wakiwa tayari kwa ajili ya kukabidhi vifaa hivyo, Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, pamoja na ujumbe wake kabla ya kukabidhi misaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko mkoani, Morogoro, Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akimshukuru Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, baada ya kumkabidhi msaada wa vitu hivyo jijini jana. Vifaa hivyo ni pamoja na mabati, vyakula, nguo na magodoro, vyenye thamani ya sh. milioni 141.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akikabidhiwa vyakula na vifaa mbalimbali na Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwashukuru viongozi wa taasisi za dini baada ya kumkabidhi vifaa hivyo, Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa taasisi hizo, Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa taasisi hizo, Dar es Salaam wakati wa makabidhiano hayo jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na wajumbe wa taasisi hizo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwakuru wanajumuiya hao.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwakuru wanajumuiya hao wa taasisi hizo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, akimweleza jambo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel pamoja na ujumbe wake, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.














Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel pamoja na ujumbe wake, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla hiyo., Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Patel Brotherhood, Subhash Patel, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wanajumuiya za dini na Taasisi ya Patel Brotherhood, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi misaada kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa ajili ya waathirika wa mafuriko, mkoani Morogoro, Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment