Monday, February 3, 2014

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala afungua kikao kazi cha Maofisa Habari na Mawasiliano


Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano waliohudhuria kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano kinachoendelea Mkoani 
Tanga, wakisikiliza maelezo na hotuba iliyokuwa ikitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. Elisante ole Gabriel.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na 
Michezo Prof. Elisante ole Gabriel akiongea na Maafisa Habari na 
Mawasiliano wakati wa Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasilianounaoendelea mktoani Tanga, ambapo amewataka kuendelea kutekelezamajukumu yao kwa ufanisi.
Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano wakiwa kimya kwa 
ajili ya kuwakumbuka baadhi ya wanataaluma ya habari waliotangualia mbele ya haki, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Leo Mkoani Tanga.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela 
Mukangara akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano (hawapo 
pichani) na kuwataka kuendelea kutumia mitandao ya kijamii katika kuwasiliana na wananchi, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Leo Mkoani Tanga. kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fennela 
Mukangara akiteta jambo na Kaimu Mhariri Mtendaji Mkuu wa Magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel Nderumaki (aliyesimama), wakati wa Kikao kazi cha Maofisa Habari na Mawasiliano Leo Mkoani Tanga. Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko na Mwisho ni kulia ni Afisa Mkuu Mawasiliano toka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bw. Peter Millanzi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene akiteta jambo na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa 
Habari na Mawasiliano wa Serikali Leo Mkoani Tanga. 
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela 
Mukangara akiwa katika picha ya Pamoja na Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakati wa ufunguzi wa wa Kikao kazi cha Maofisa Habari na Mawasiliano Leo Mkoani Tanga.Kushoto kwa waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene na mwisho kushoto ni Afisa Mkuu Mawasiliano toka Mamlaka ya Usimamizi wa BandariTanzania(TPA) Bw. Peter Millanzi. Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko akifuatiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari( MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa na mwisho kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Simwanza.

Frank Mvungi- Maelezo

SERIKALI imesema haina Ugomvi na vyombo vya habari hapa nchini kama ambavyo baadhi ya vyombo  hivyo vimekuwa vikiripoti.

Akizungumza leo, katika ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano  wa Serikali Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara alisema haoni sababu ya kuingia kwenye ugomvi na wadau muhimu kama vyombo vya habari.

“Kuna wanaozunguka zunguka wakieleza kwamba kuna ugomvi kati yetu na vombo vya habari, mkiwasikia wapuuzeni”.alisema waziri Mukangara.

Dkt Mukangara alipongeza kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya habari na kuvitaja kuwa wadau muhimu wa Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na kutoa taarifa.

Dkt.Mukangara aliongeza kuwa ni jukumu la Maafisa Habari na Mawasiliano kuwaunganisha wananchi na Serikali kwa kutoa taarifa zitakazowasaidia wananchi kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akifafanua zaidi Dkt. Mukangara amesema kuwa Wizara itaendelea kuratibu mikutano ya Taasisi za Serikali na Vyombo vya Habari ili kuwapa wananchi fursa ya kujua mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.

Katika Utaratibu huo  Dk Mukangara amesema mikutano 156 kati ya taasisi za Serikali na Vyombo vya Habari ilifanyika  kati ya 204 iliyotarajiwa kufanyika katika kipindi cha julai hadi Desemba 2013 ikiwa ni utekelezaji wa jukumu la msingi la kuwapa wananchi taarifa kwa wakati.

Pia aliwaasa Maafisa Habari na Mawasiliano kote nchini kujituma na kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia Taifa kufikia maendeleo endelevu.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel Alibainisha kuwa Mafunzo kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.,mafunzo ya vitendo kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii na mada kuhusu namna bora ya kutumia na kuendesha radio za kijamii.

Kauli mbiu ya Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano zaidi ya 100 toka Tanzania nzima ni Matumizi ya Tehama na Mitandao ya Kijamii katika kuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa umma.

No comments:

Post a Comment