Friday, March 7, 2014

Kikao cha Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo wajumbe wenzie Bi. Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Richard Ndassa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, kabla ya kuingia katika Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
(Picha zote na Hassan Silayo- Maelezo na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli akimweleza jambo Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo Bw. John Mnyika Mapema leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Ismail Aden Rage (mwenye kanzu) na Hashim Rungwe wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Fathiya Zahran (kulia) na Salam Said (wa pili kulia), wakizungumza na wageni wao, Tatu Kano (kushoto) na Alya Riyami (wa pili kushoto), walipowatembelea viwanja vya Bunge, mjini Dodoma leo. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka kushoto) Jaku Ayoub, Ali Vuai na Kibanda, wakielekea kwenye ukumbi wa bunge kwa ajili ya kuanza kikao cha kujadili Rasimu ya Kanununi za bunge hilo leo asubuhi.  
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anna Kilango (kushoto), akijadili jambo na mjumbe mwenzake wa bunge hilo, Easter Bulaya wakati wakielekea kwenye ukumbi wa bunge kwa ajili ya kikao cha kujadili Rasimu ya Kanuni za bunge hilo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohammed Seif Khatib na Anna Makinda (Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa kikao hicho leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohamed Seif Khatib (kushoto), Anne Makinda, wakizungumza jambo kwenye ukumbi huo leo asubuhi. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakizungmza na simu kabla ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, kuanza kikao cha asubuhi leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anna Makinda (Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimweleza jambo, mjumbe mwenzake wa bunge hilo, Vicky Kamata, kabla ya kuanza kwa kikao hicho leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwaeleza jambo wajumbe wa Bunge maalum la Katiba Edward Lowassa (mwenyeshati Jeupe) na Philemon Ndesamburo, Ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, SheikhThabit Noman Jongo akiongoza dua ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo, Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Mstaafu Donald Mtetemelaakiongoza sala ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma. 

No comments:

Post a Comment