Saturday, May 17, 2014

40 wauawa kwa shambulizi Benghazi

Waziri Mkuu wa Libya Abdallah Al thinni amekuwa akisisitiza kuwa serikali haikuamuru kuhusu shambulio hilo
Wizara ya afya nchini Libya imesema zaidi ya watu 40 wameuwawa mjini Benghazi siku ya  Ijumaa katika mashambulizi ya anga na nchi kavu yaliyoongozwa na kanali wa zamani wa jeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislam.
Vurugu hizo zilizofanyika zinaelezwa kuwa zilikuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu mapinduzi ya yaliyomuondoa madarakani Kanal Muamar Gadafi mwaka 2011.

Mtu aliyeogoza mashambulizi hayo, Khalifa Haftar amesema ataendelea na kampeni yake ya kuwaondoa watu wote aliowaita magaidi nje ya mji wa Benghazi.Taarifa kutoka mjini Benhgazi zinasema hivi sasa utulivu umerejea kwenye mji huo kama ilivyokuwa awali.
Serikali kuu imelaani matumizi hayo ya nguvu na kuuita hatua hiyo kama jaribio la mapinduzi lililoshindwa.

No comments:

Post a Comment