Sunday, August 24, 2014

MAFANIKIO YA OPARESHENI ENDELEVU KATIKA JIJI LA DR ES SALAAM KUANZIA 11/08/2014 hadi 20/08/2014




Operesheni dhidi ya wahalifu inayoendelea katika katika jiji la Dar es Salaam imekuwa na mafanikio makubwa , kwani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 11/08/2014 hadi tarehe 20/08/2014 jumla ya watuhumiwa kumi na wanane (18) wamekamatwa katika Operesheni hiyo na miongoni mwa watuhumiwa hao wamo wanawake watatu (3).

Watuhumiwa waliokamatwa wanahusika na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha, mauaji na wizi wa magari. Aidha baadhi ya watuhumiwa wamekamatwa wakiwa na vielelezo vilivyotumika katika matukio ya uhalifu na vielelezo vilivyoibwa katika matukio.



Watuhumiwa waliokamatwa katika Operesheni hii inayoendelea ni pamoja na:-

1.      Chacha S/O Mwita @ Sura Bin Sura, 43yrs, Mngurumi, mkazi wa tegeta kwa Ndevu.

2.      Dadi S/O Kaisi Mshamu, 29yrs, Mmakonde, mkazi wa Yombo Vituka.

3.      Yusuph S/O Selemani @ Mlanzi, 26yrs, Mndengereko, mkazi wa Yombo Kilakala.

4.      Fatuma D/O Mussa Mlawaja, 39yrs, Mzaramo, mkazi wa Kitunda Mzinga.

5.      Athanasi S/O Meja Kivike, 31yrs, Mhehe, dereva Bodaboda na mkazi wa Mwananyamala kwa mama Zakaria.

6.      Kassa S/O Ibrahim Lusama, 39yrs, Mzaramo, mkazi wa Kitunda.

7.      Alex S/O Anyimile Mwandemele @ Babu, 38yrs, Mnyakyusa, mfanyabiashara, mkazi wa Ukonga Karakata.

8.      Judith D/O Aminiel @ Judy , 36yrs, Mchaga, mfanyabiashara, mkazi wa Mwananyamala.

9.      Irine D/O Muro, 35yrs, Mchaga, mfanyabiashara, mkazi wa Mwananyamala.

10.  Saidi S/O Iddi Nangunda @ Papasi, 40yrs, Mzaramo, Dereva, mkazi wa Mbagala.
11.  Anthony S/O Godwin, 40yrs, Myao, mfanyabiashara,    mkazi wa Kinondoni ‘A’

12.  Abdallah S/O Iddi Nyamgunda @ Mpemba, 35yrs, Mzaramo, Dereva na mkazi wa Kinondoni Mkwajuni.

13.  Gethe S/O Benjamin @ Benja ,32yrs, Mnyaturu, mfanyabiashara, mkazi wa Vingunguti.

14.  Twalib S/O Hashim Nkya @ Osaka, 53yrs, Mchaga, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi Luis.

15.  Yusuph S/O Hashim Nkya, 48yrs, Mchaga, mfanyabiashara, mkazi wa Salasala.

16.  Juma S/O khamis Hussein @ Kipara, 31yrs, Muha, mfanyabiashara, mkazi wa Mbagala Mission.
17.  Edward S/O Rajabu, 32yrs, Muha, mafanyabiashara, mkazi wa Tegeta.

18.  Mohammed S/O Chelewa, 31yrs, Mmwera, Dereva wa Bodaboda, mkazi wa Mwananyamala.

Matukio mbalimbali waliyoshiriki au waliyohusika nayo watuhumiwa hawa ni kama ifuatavyo:-

1.      Mnamo tarehe 14/08/2014 huko Karakata mtuhumiwa Fatuma D/O Mussa Mlawaja alipatikana na Bastola moja yenye namba za usajili AB. 221321, risasi 15 za Bastola na magazine mbili (2) za Bastola. Mtuhumiwa huyu ni ndugu wa Jambazi Sugu aitwaye Jumanne S/O Mohammed @ J4, ambaye bado hajakamatwa

2.      Mnamo tarehe 14/06/2014 majira ya saa 13:10hrs huko maeneo ya Leadres Club Kinondoni, jirani na kampuni ya ulinzi ya Ultimate, watuhumiwa Chacha S/O Mwita @ Sura Bin Sura, Said S/O Kaisi Msham, Yusuph S/O Selemani  @ Mrazi , Athanas S/O Meja Kivike, Kassa S/O Ibrahim Lusama, Alex S/O Anyimile Mwandemele @ Babu, Jumanne S/O Mohammed @ J4 na Abdul @ Chozi ambao bado hawajakamatwa walimpora Nina D/O Stanslaus Bwagaya fedha taslim Tshs 10,000,000/= wakitumia Bastola aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Fatuma D/O Mussa Mlawaja. Watuhumiwa wamekiri kuhusika na tukio hilo na wanaendelea kuhojiwa

3.      Mnamo tarehe 13/08/2014 majira ya mchana huko Yombo Vituka wakati wa ukamataji mtuhumiwa Dadi S/O Kaisi Mshamu alikamatwa akiwa nna mlipuko mmoja wa Bomu.

4.      Mnamo tarehe 20/08/2014 majira ya mchana saa 20:30hrs huko Mbagala Saba Saba, alikamatwa Juma S/O Hussein @ Kipara na alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na silaha aina ya SMG yenye namba za usajili AU-4443 – 1997 na risasi 152 pamoja na Magazine tupu mbili (2).

5.      Mnamo tarehe 04/08/2014 majira ya saa 19:00hrs huko Mwananyala kwa Mama zakaria jirani na Mahamo Bar, majambazi watatu wakiwa na SMG waliokuwa na pikipiki moja walipora fedha taslim Tshs 2,000,000/= na kisha wakifyatua risasi na kusababisha vifo vya Nestory S/O Tarimo na Jeremiah S/O Tarimo. Katika eneo la tukio yaliokotwa maganda matatu ya risasi za silaha aina ya SMG. Watuhumiwa Juma S/O Hamis @ kipara, Edward S/O Rajab Keleye na Mohammed S/O Chelea, wamekiri kuhusika na mauaji hayo.

6.      Mnamo tarehe 11/08/2014 majira ya saa 22:15hrs huko maeneo ya Victoria majambazi watano wakiwa na bunduki aina ya SMG wakitumia pikipiki mbili, walipora pikipiki Na: T.283 CSX aina ya Kapor rangi nyeusi na kumjeruhi kwa risasi dereva wa Boda boda aitwaye Abuu S/O Ayubu. Watuhumiwa Juma S/O Hamis @ kipara, Edward S/O Rajab Keleye na Mohammed S/O Chelea wamekiri kuhusika na tukio hilo.

7.      Mnamo tarehe 13/08/2014 majira ya saa 21:30hrs huko Sinza katika Duka la M-Pesa na Tigo – Pesa majambazi wanne wakiwa na pikipiki mbili walivamia duka hilo na kumjeruhi kwa risasi nmmiliki wa duka hilo aitwaye Elisha Mosha na Kisha kupora fedha Tshs 300,000/=. Watuhiwa Juma S/O Khamis Hussein @ Kipara, Edward S/O Rajab Keleye na Mohammed S/O Chelea, wamekiri kuhusika na tukio hilo.

8.      Mnamo tarehe 07/08/2014 majira saa 23:00hrs huko Mikocheni B katika Bar ya Kabile, Majambazi wapatao sita (6) wakiwa na SMG wakitumia pikipiki mbili (2) walifyatua risasi na   kupora fedha taslim Tshs 1,400,00/= toka kwa Mussa S/O Shaban. Watuhumiwa  Juma S/O Khamis Hussein @ Kipara, Edward S/O Rajab Keleye na Mohammed S/O Chelea, wamekiri kuhusika na tukio hilo.

Aidha katika Operesheni hii juumla ya magari  sita (6) yamekamatawa, magari hayo yameripotiwa kuibwa toka sehemu mbalimbali hapa Jijini. Orodha ya magari hayo ni kama ifuatavyo:-

1.      T. 743 CGP Toyota RAV 4 rangi ya Silver.
2.      T. 229 BYE Toyota OPPA, rangi ya silver.
3.      T. 836 CBB Toyota VOXY, rangi nyeusi.
4.      T. 323 BTV  Toyota IST, rangi ya Silver.
5.      T. 249 CEP Toyota MARK II GX 110, rangi ya silver.
6.      T. 216 CHe Toyota NOAH, rangi Nyeusi.

·         Kwamba gari T. 743 CGP Toyota RAV 4 amekutwa nayo mhutumiwa Gethe S/O Benjamin @ Benja, gari hili limeripotiwa kuibwa maeneo ya Mikocheni ‘B’

·         Kwamba gari T. 229 BYE Toyota OPPA, amekamatwa nayo mtuhumiwa Gethe S/O Benjamin @ Benja, gari hili limeripotiwa kuibwa katika Show Room ya Africariers iliyopo barabara ya Nyerere.

·         Kwamba gari T. 836 CBB Toyota VOXY, amekamatwa nayo mtuhumiwa Gethe S/O Benjamin @ Benja, gari hili limeripotiwa kuibwa kwenye Yard ya magari iliyopo eneo la Morocco .

·         Kwamba gari  T. 323 BTV  Toyota IST,   amekamatwa nayo dalali aitwaye Twalib S/O Hashim Nkya @ Osaka,  gari hili limeripotiwa kuibwa katika Yard ya magari iliyopo eneo la  Morocco .

·         Kwamba gari  T. 249 CEP Toyota MARK II GX 110,   amekamatwa nayo dalali aitwaye Yunus  S/O Hashim Nkya   gari hili limeripotiwa kuibwa katika Show Room ya Africariers iliyopo barabara ya Nyerere.

·         Kwamba gari  T. 216 CHe Toyota NOAH,   amekamatwa nayo dalali Elius S/O Yahaya  Mwadi, gari hili limeripotiwa kuibwa nyumbani kwa Mohammed S/O Mwinyi na watuhumiwa wengine waliokamatwa kuhusiana na tukio hili ni Judith D/O Aminieli @ Judy, Irine D/O Murro, Saidi S/O Iddi Nangunda @ Papasi, Anthony S/O Godwin na Abdallah S/O Iddi Nyamgunda.

Pia kaika Operesheni hiyo polisi Mkoa wa Kinondoni walifanikiwa kuokoa fedha taslim Tshs 51,689,000/= zilizodaiwa kuporwa  katika tukio la ujambazi  kwenye  kituo cha mafuta cha Gudal Kilichopo Ubungo River side. Watuhumiwa waliohusika na tukio hilo ni Saad S/O Mohammed, Edwin S/O Abdon  na Zurehabi D/O Yusuph. Hata hivyo kilichobainika katika tukio hili ni kwamba tukio hili lilikuwa la kutengeneza kwani fedha hizo zilikuwa tayari zimeshachukuliwa kabla ya tukio halijafanyika na waliobainika kuhusika na tukio hilo ni wafanyakazi wa kituo hicho ambao majina yao ni kama yalivyo ainishwa hapo juu. Ambao wote wameshafikishwa Mahakamani.

No comments:

Post a Comment