Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu
saba wanaotengeneza noti bandia za Dolla ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza
katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Watuhumiwa hao
walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola
mia (100) ambazo ni sawa na DOLLA 1,064,000 (Dolla Millioni Moja na Sitini na Nne Elfu) sawa na shilingi za
kitanzania 1,702,400,000/= (TSH.
Billioni Moja, Millioni Mia Saba na Mbili na Laki Nne) katika nyumba namba
07 walimokuwa wamepanga.
Polisi walipata
taarifa toka kwa wasamaria wema na kuweka mtego wa kuwakamata ndipo askari
walipofika eneo hilo waliwakamata watuhumiwa na noti za USD bandi zikiwa
zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo imefungwa kwa namba za siri.
Aidha watuhumiwa hao walikiri kujihusisha
na utengenezaji wa noti bandia, watuhumiwa hao ni kama ifuatavyo;
1.AHMAD S/O MOHAMED
Miaka 50, mfanyabiashara, mkazi wa Mombasa Kenya
2.ICHARD S/O MAGOTI
Miaka 61, mfanyabiashara, mkazi wa Musoma mkoani Mara.
3.SIMONI S/O LUKIKO
Miaka 58, mkazi wa Magomeni Kagera
4.HUMPREY S/O
LEONARD Miaka 34, mlinzi, mkazi wa Mburahati
5.FRANK S/O CHARLES
Miaka 31 mfanyabiashara, mkazi wa Sinza
6.ABDALLAH S/O
YUSUPH, Miaka 34, mfanyabiashara, Mkazi
wa Sinza
7.BAKARI S/O BAKARI, Miaka 31, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi, Kimara.
Aidha watuhumiwa
hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani
kwa hatua zaidi za kisheria.
KUPATIKANA KWA BHANG GUNIA TATU (3), GONGO LITA 600 NA
WATUHUMIWA
Aidha katika tukio lingine
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeendelea kufanya operesheni na
limefanikiwa kukamata watuhumiwa watano wakiwa na gunia tatu za dawa za kulevya
aina ya Bhang na Gongo lita 600 na mitambo sita ya kutengenezea pombe hiyo
haramu ya Moshi
No comments:
Post a Comment