Tuesday, May 19, 2015

MJi wa Ramadi wasalia bila watu

Maelfu ya raia wa Iraq wanaendelea kuukimbia mji wa Ramadi huku kundi la wanamgambo wa Islamic State likiwazuia na kuendeleza mashambulizi ya kuudhibiti mji wa Ramadi.
Waasi hao wameuteka mji huo kutoka kwa vikosi vya serikali.
Umoja wa mataifa unasema kuwa watu elfu 25 wameutoroka mji huo katika siku kadhaa zilizopita, wakielekea mashariki hadi mjini Baghdad.
Raia wapatao elfu mia moja na thelathini walitoroka mji huo mwezi uliopita, ulipovamiwa na kundi la Islamic State.
Shirika la umoja wa mataifa pamoja na mashirika mengine, yameanza kusambaza chakula, maji na dawa, huku pia kambi za muda zikijengwa.

No comments:

Post a Comment