Rais wa Afrika ya kusini Jacob Zuma amekuwa kiongozi wa hivi karibuni anayetaka uchaguzi wa urais nchini Burundi kuahirishwa.
Akizungumza baada ya mkutano wa kieneo
nchini Angola,Bwana Zuma alisema kuwa uchaguzi huo haupaswi kufanyika
hadi hali ya amani itakaporudi nchini humo.
Maandamano yanaendelea katika mji wa Bujumbura kufuatia jaribio la mapinduzi la wiki iliopita.
Rais wa taifa hilo amekana madai ya kutaka kulipiza kisasi dhidi ya watekelezaji wa shambulio hilo.
Wafanyikazi wa mahospitali nchini
Burundi awali walielezea kuwa kumekuwa na mshambulizi ya kulipiza kisasi
ambapo polisi wamekuwa wakiwajeruhi wanajeshi waliodaiwa kuhusika na
jaribio hilo.
No comments:
Post a Comment