Miripuko na milio ya risasi ilisikika katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, usiku wa jana ambapo watu wawili wanaripotiwa kuuwawa masaa machache kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa katika uchaguzi unaofanyika leo.
Hali ya ukosefu wa utulivu inakuja kutokana na wasiwasi kuhusiana na juhudi zenye utata za Rais Pierre Nkurunziza kutaka kuchaguliwa tena kwa kipindi cha tatu, ambapo waandamanaji wamesema nia yake hiyo inakiuka katiba, ambayo inaruhusu ukomo wa vipindi viwili.
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa leo asubuhi kwa ajili ya uchaguzi huo ambao unasusiwa na vyama vikuu vya upinzani na kutishia kuitumbukiza nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika ghasia kubwa. Zaidi ya raia 160,000 wa Burundi wamekimbilia nchi jirani, wengi wakisema wanahofia mashambulizi ya vijana wa chama tawala wanaojulikana kama Imbonerakure
No comments:
Post a Comment