Mkuu
wa gereza la Karanga, mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, ambako ndiko
kilipo kiwanda cha kutengeneza viatu, Kamishna Msaidizi wa Magereza,
(ACP), Hassan Bakari Mkwiche, (kushoto), akionyesha kitu, wakati
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (wakwanza
kulia), alipotembelea kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa
ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa cha viatu, Oktoba 9, 2016. Wengine
pichani ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (wapili
kushoto), Mkuu wa magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa
Polisi, (ACP), Anderson Kamtera.
Bw.
Erio, na maafisa wake, wakipatiwa maelezo na maafisa wa Jeshi la
Magereza alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa
kiwanda hicho.
NA
K-VIS MEDIA, Moshi
MKURUGENZI
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, ametembelele kiwanda cha
kutengeneza viatu cha Karanga mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Oktoba 9, 2016,
ili kuona eneo ambalo kitajengwa kiwanda kipya na cha kisasa.
Bw.
Erio ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Steven
Alfred, na Meneja Uhusiano, Bi.Lulu Mengele, pia alipata fursa ya kupokea
taarifa ya uendeshaji wa kiwanda cha sasa na changamoto zinazokikabili.
Bw.
Erio alisema, ziara yake inalenga kujua mambo mawili ambayo ni kuona eneo
patakapojengwa kiwanda kipya cha kutengeneza bidhaa za ngozi, lakini pia kupata
uelewa wa nini kifanyike ili kuboresha kiwanda cha sasa ambacho kilijengwa
mwaka 1977.
Maafisa
wa kiwanda hicho, walimuonyesha maeneo mawili ambayo yanafaa kujengwa kiwanda
hicho.
“Kama
mtakumbuka, wiki iliyopita mimi na Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), John
Minja tulisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya PPF na Jeshi la Magereza katika
kukiboresha kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga, lakini pia kujenga
kiwanda cha kisasa cha kuchakata ngozi na kutengeneza bidhaa zitokanazo na
ngozi.” Alianza kwa kusema.
Alisema,
nia ya Mfuko ni kuona kazi ya ujenzi wa kiwanda kipya inakamilika ifikapo
Desemba 2018 ili kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi
wa viwanda.
“Wakati
tukisubiri ujenzi wa kiwanda kipya ukamilike, lazima pia tuboreshe hiki cha
sasa kwa kuimarisha miundombinu iliyopo, na hivyo kuongeza uzalishaji na kupanua
masoko ” alisema Bw. Erio.
Aliagiza
wataalamu wa PPF kwa kushirikiana na wenzao wa Magereza (kiwanda cha Karanga),
wakutane haraka ili kuainisha chamngamoto zinazokikabili kiwanda cha sasa, ili
uboreshaji wa mitambo uweze kufanyika kwa haraka.” Alifafanua.
Awali
Kaimu Mkuu wa kiwanda cha viatu Karanga, Naibu Mrakibu wa Magereza,( ASP),
Michael Minja, alisema kiwanda cha sasa kinakabiliwa na changamoto nyingi,
ikiwa ni pamoja na uchakavu wa mitambo, ambapo alisema baadhi ya mashine
zimepitwa na wakati na zingine zimeharibika na hivyo zinahitaji kufanyiwa
ukarabati mkubwa.
“Mambo
yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kuwezesha uendeshaji bora wa kiwanda, ni pamoja
na kununua vipuri kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya mashine, lakini pia kuna
upungufu wa baadhi ya mashine hivyo tunahitaji kuongeza idadi yake.” Alisema
ASP Minja.
Akizungumza
kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, (CP), Editha
Malya, alisema, Jeshi la Magereza limefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na
PPF katika kushirikiana katika uendeshaji wa kiwanda cha viatu Karanga ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya na cha kisasa.
“Tutashirikiana
kwa karibu ili kuhakikisha azma yetu inatimia kwa haraka,” alisema CP Malisa.
Kiwanda
cha viatu Karanga, kilichoko kwenye eneo la Gereza la Karanga mjini Moshi,
kilizinduliwa na Rais wa awamu ya kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,
Juni 3, 1977 na wateja wakubwa wa bidhaa
za kiwanda hicho ni taasisi cha kijeshi, ikiwa ni pamoja na JWTZ, JKT, Magereza
na Jeshi la Polisi.
Kamishna
wa Magereza, (CP), Editha Malya, aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la
Magereza Nchini, (CGP), akizungumza wakati wa kikao cha kupeana taarifa
na ujumbe wa PPF ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Erio Oktoba 9, 2016
Bw. Erio, akizungumza wakati wa mkutano huo mfupi kabla ya kukagua maeneo hayo ya ujenzi.
Mkurugenzi
wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (katikati), akizungumza jambo
wakati wa mkutano huo. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu
Mengele, na kushoto ni Kamishna wa Magereza, Editha Malya.
Kaimu
Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga, Mrakibu Msaidizi wa
Magereza, (ASP), Michael Minja, akitoa taarifa ya utendaji wa kiwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred, wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo.
Bw. Erio(kushoto), akiangalia moja ya viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo.
Mkurugenzi
wa Uwekezaji wa PPF, Bw. Steven Alfred, akionyeshwa namna kiatu
kinavyotengenezwa, (katikati) ni mwakilishi mkuu wa ofisi ya PPF mkoani
Kilimanjaro, Bw. Jacob Cornel Sule.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred,
wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo. Kushoto ni Mkuu wa
Gereza la Karanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP), Hassan Bakari
Mkwiche.
Mkuu
wa kitengo cha umeme wa Kiwanda cha viatu Karanga, Staff Surgent,
Aulelia Mushi, akziungumzia mahitaji ya umeme kiwandani hapo.
Maafisa wa wa Jeshi la Magereza, wakisikiliza mazungumzo hayo.
Picha ya Pamoja baada ya kutembelea kiwanda.
Ukaguzi wa moja ya maeneo ya ujenzi wa kiwanda.
Jiwe la msingi aliloweka Mwalimu Nyerere wakati wa ufunguzi wa kiwanda Juni 3, 1977.
Meneja
Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (watatu kushoto), akiangalia moja ya
viatu vinavyotengenezwa kiwandani hapo, Kushoto ni Kamishna wa
Magereza, Editha Malya, Mwakilishi Mkuu wa PPF, Mkoani Kilimanjaro,
Jacob Cornel Sule, Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, (RPO), Kamishna
Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtera, na maafisa wengine.
Bw. Erio akisalimiana na Kamishna wa Magereza, Editha Malya.
No comments:
Post a Comment