Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akikagua mradi wa kituo
cha kutibu maji taka kilichopo Hamkoko wilayani Ukerewe, mwenye fulana
ya michirizi ni mhandisi mshauri wa mradi huo Mhandisi Edward Kazimoto
na kushoto mwenye kofia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.Nyuma
kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi wa MWAUWASA Mhandisi Anthony Sanga.
Picha Na Baltazar Mashaka.
Mhandisi
mshauri wa mradi wa Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria (LVWATSAN)
mhandisi Edward Kazimoto kitoa ufafanuzi wa ramani (michoro) ya miundo
mbinu ya chanzo cha Maji Nebuye na kituo cha kutibu maji taka cha
Hamkoko kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (mbele)
mwenye shati la mchanganyiko wa rangi.Kusjhoto mwenye suti ya rangi ya
kahawia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mwauwasa Mhandisi Anthony Sanga.
Mhandisi
mshauri wa mradi wa Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria (LVWATSAN) Ukerewe
(kushoto)mhandisi Edward Kazimoto juzi akimwongoza Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kukagua miundombinu ya chanzo cha
maji Nebuye kushoto kwa waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomihn
Chang'ah na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mwauwasa Mhandisi Anthony Sanga
. Na Baltazar Mashaka
Waziri
wa maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akionyeshwa sehemu ya
mabawa wa ya kupokelea maji kabla ya kutibiwa na kusafishwa kabla ya
kusukumwa kwenye tanki la kuhifadhia maji katika chanzo cha Nebuye.
Kutoka kulia wa pili ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomihn Chang'a. Na
Baltazar Mashaka.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akiangalia mitambo ya
kusukuma maji katika chanzo cha Maji Nebuye wilayani Ukerewe
juzi.kushoto ni mhandisi mshauri wa mradi wa Usafi wa Mazingira Ziwa
Victoria (LVWATSAN) mhandisi Edward Kazimoto. Na Baltazar Mashaka
NA BALTAZAR MASHAKA,NANSIO UKEREWE
WAZIRI
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amewakemea Watumishi wa
umma wasiowajibika na wanaofanya kazi kwa mazoea kuwa watafute mlango wa
kutokea kwa kuwa wamekuwa chanzo cha kufa kwa miradi mingi ya serikali.
Pia
waziri huyo alisema hakuna maji ya bure na kuwataka wananchi Ukerewe
kuchangia gharama za huduma ya maji watakayoyatumia baada ya kukamilika
kwa mradi wa Maji Nansio ili uwe endelevu na kuwawezesha watu wengine wa
serikali na binafsi kupata huduma hiyo.
Mhandisi
Lwenge alisema juzi mjini Nansio Ukerewe alipozungumza na baadhi ya
wananchi, wadau na watumishi wa idara za Halmashauri ya Wilaya ya
Ukerewe kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo mara baada ya kukagua chanzo
cha maji Nebuye na kituo cha huduma ya majitaka Hamkoko.
“Mradi
huu wa Maji Nansio na kituo cha maji taka ambao umegharimu bilioni 13
ni mzuri ni wa pekee nchini.Wengine watakuja kujifunza hapa na utakuwa
na uwezo wa kuzalisha lita milioni 8 za maji kwa siku licha ya
changamoto ya uhaba wa wahandisi wa ujenzi, umeme na mitambo,” alisema
Mhandisi Lwenge.
Waziri
huyo wa Maji alisema serikali imedhamiria kuwa ifikapo mwaka 2020
asilimia 100 ya wananchi wa Ukerewe wapate maji safi na salama kwa
maeneo mengine asilimia 85 na hivyo kazi ya mazoea imepitwa na wakati.
“
Tunalo deni kwa waliotuchagua baada ya kuona ilani inatekelezeka.Kazi ya
mazoea imepitwa na wakati,watumishi ambao hawatawajibika watafute
mlango wa kutokea kwa sababu miradi mingi ya serikali inakufa kutokana
na watendaji kutowajibika.Tuutunze miradi huu uwe endelevu,”alisema
Lwenge.
Waziri
huyo wa maji alieleza kuwa majungu hayasaidii ila atakayefanya ya ovyo
watu waseme kwani ili kuwekana sawa kuelekea kwenye maendeleo ya Wilaya
ya Ukerewe na kuomba ushirikiano katika kuwaongoza wananchi walioipigia
kura nyingi serikali ya CCM .
Alisema
kuwa chama ( CCM ) kianze kuisimamia serikali ili irudi kwenye misingi
kwa sababu inawajibika kwa wananchi kma hawachangii maendeleo katika
maeneoe yao hapo kuna tatizo na lazima kiongozi wa hapo aulizwe.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomihn Chang’ah alisema mradi huo una
manufaa makubwa kwa wananchi wa Nansio na wilaya hiyo na asilimia 70
watanufaika kwa kupata huduma ya maji safi na salama na inahitaji sh.
milioni 533,600,000 ili Mamlaka ya Maji Nansio imudu kuuendesha.
Alieleza
kuwa fedha hizo ni za nishati ya umeme wa kuendesha mitambo, manunuzi
ya dawa ya kutibu maji,dira za maji,mabomba na viunganishi na mishahara
ya watumishi watakaosimamia mradi huo kwa mwaka .
“Mradi
huu ni mkubwa kulinganisha na uwezo wa sasa wa rasilimali fedha wa
mamlaka, Serikali kupitia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira
Mkoa wa Mwanza (MWAUWASA) tunaomba itupatie mtaji wa sh. 533,600,000
,”alisema Chang’ah.
Aidha,
mshauri wa mradi huo Mhandisi Edward Kazimoto alisema kuwa kasoro
alizoelezwa waziri walishaziona na kuzirekebisha na kazi kubwa iliyobaki
ni halmashauri kuwafungia wananchi dira za maji ili waanze kupata
huduma hiyo.
Mradi
huo wa Maji Nansio umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
pamoja na serikali kwa gharama ya Bilioni 13 na kutekelezwa na
mkandarasi kampuni ya Angelique International Limited ya India.
No comments:
Post a Comment