Rais wa Marekani Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais, baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yalioafikiwa na mtangulizi wake Barak Obama.
Muda mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake, Bw Trump, alitia amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu inayofahamika kama Obamacare, ambayo Trump aliahidi kufanyia marekebisho.
Trump pia ametia saini amri ya kuwaidhinisha mawaziri wake wapya wa Ulinzi na usalama wa kitaifa ambao uteuzi wao umepitishwa na bunge la seneti.
Utawala wa Trump pia umeaanza kufanyia marekebisho mtandao wa kijamii wa Ikulu ya White House kwa kuweka masuala yatakayopatiwa kipaumbele na uongozi huo mpya.
No comments:
Post a Comment