Mwenyekiti
wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia Mhe. Balozi Ombeni Sefue (wa pili
kushoto) akipokea kompyuta kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini
Mhe. Song Geum Young, wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Muombwa
Mwinyi na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia Dkt.
Bernard Archiula.
Mhe.
Balozi Sefue akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Bodi na Uongozi wa
Chuo cha Diplomasia mara baada ya kupokea ufadhili huo kutoka kwa
Serikali ya Jamhuri ya Korea.
Balozi
Mwinyi akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki ambapo aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa
kuendelea kuwa mdau wa maendeleo katika sekta mbalimbali nchini hususan
sekta ya Elimu.
Sehemu
ya Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo
pichani) wakati alipokuwa anatoa neno la shukrani.
Sehemu nyingine ya watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakishuhudia makabidhiano.
Dkt. Bernard Archiula (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa Balozi Sefue na Balozi Mwinyi.
Balozi
Ombeni Sefue akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi
Kasiga.
Wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment