Meneja
Chapa wa Tigo, William Mpinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kifurishi
kisicho isha muda cha halichachi. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo,
Woinde Shisael.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Tigo Tanzania leo imetangaza kuanzishwa kwa ubunifu mwingine wa
kifurushi cha data na sauti ili kukabiliana na hitaji la wateja.
Kifurushi kipya kinajulikana kama ‘Halichachi’ (Muda wake hauishi) na ni
mwendelezo wa kujikita kwa Tigo katika kuwapatia wateja wake uhuru
wa mawasiliano.
Akizungumza
katika mkutano wa waandishi wa habari leo wakati akitangaza kampeni
hiyo mpya Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga alisema, “Tuna furaha
kubwa wakati kampuni inazindua kifurushi kipya ambacho
kitawahakikishia wateja wake kwamba wanakuwa na mamlaka ya kumiliki
vifurushi vyao wakati muda wa kumalizika kwa kifurushi haitakuwa ni
changamoto tena.”
“Ni
dhahiri kuwa soko la mawasiliano ya simu linakua ambapo huduma za
mawasiliano ya simu za mkononi zinaongezeka kwa mrengo wa kununua
vifurushi,” alisema Mpinga na kuongeza, “Tunazindua kifurushi cha
kipekee tukiwa tunajiamini kwamba kitakuwa ni suluhisho sahihi kwa
wateja wetu.
“Kifurushi
hiki kinaingia katika soko ikiwa ni sehemu ya mtiririko wa ubunifu
uliowekwa ili kuhakikisha kwamba tunasimamia mtazamo wetu katika kutoa
huduma nzuri kwa wateja wetu.
Tunaamini
kwamba kifurushi hiki ni kiashiria kilicho wazi kwamba tunaongoza
katika kutoa masuluhisho ya mawasiliano ya simu yaliyo na ufanisi
nchini Tanzania.”
Kifurushi
hiki kipya ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kutoa huduma ndani ya
safari yake ya ubunifu na miongoni mwake ikiwa ni kuanzishwa kwa
huduma ya bure ya WhatsApp, Facebook ya Kiswahili na YouTube ambayo
kampuni ilizindua mwaka 2016.(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment