Friday, March 10, 2017

JAJI WARIOBA AZINDUA KITABU CHA KIONGOZI MWANAMKE

 Waziri mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba akionesha kitabu juu mara baada ya kuzindua kitabu cha Mwanamke kiongozi katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
 Aisha Bdel na Liliani Lihundi wakifurahi mara baada ya Jaji wa Rioba kuzindua kitabu cha Mwanamke kiongozi
 Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza na Wanawake waliofika katika kongamano la Wanawake na Wasichana  juu ya uongozi ndani ya Tanzania na kuzindua kitabu kinachohusu Mwanamke
 Dkt Mwele Malecela akizungumza juu ya mambo aliyojifunza wakati anagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi na kuwataka wazazi kuwa ndio waangalizi na kuwatoa hofu wasichana pindi wanapohitaji kujaribu jambo lolote lenye manufaa kwa Jamii
 Muendesha Mjadala Liliani Lihundi akizungumza wakati wa kongamano hilo ambalo lilihusisha wasichana na wanawake
 Mbunge Viti Maaalum Chadema , Susan Lymo akichangia jambo juu ya uozefu wake kama mwanamke katika Bunge la Jamhuri wa muungano
 Waziri mkuu Mstaafu Jaji  Joseph Sinde Warioba akiwa na Mama Anna Abdalah wakiwasalimia wanafunzi wasichana wa chuo kiku cha Dar es Salaam ambao walifika katika kongamano hilo
Baadhi ya washiriki waliokaa Safu ya mbele katika kongamno hilo

DC Kanali Ndagala kuwachukulia hatua watakaoshindwa kumaliza miradi ya ujenzi wa shule kwa wakati wilayani Kakonko,mkoani Kigomamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya shule

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
 
MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala ameahidi kuwachukulia hatua wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, endapo watashindwa kukamilisha miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa muda muafaka kutokana na changamoto iliyopo ya upungufu wa vyumba vya madarasa kutatuliwa.

Maagizo hayo aliyatoa jana wakati akikagua ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili katika Shule ya Msingi Kakonko Wilayani humo, ambapo alibaini kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi kwa mafundi hali inayo pelekea kusua sua kwa ujenzi huo.

Mkuu huyo alisema mradi huo ulitakiwa kuwa umekabidhiwa, lakini mpaka sasa bado haujakamilika kutokana na uzembe wa baadhi ya wasimamizi Wa mradi huo kushindwa kuwasimamia mafundi ipasavyo waweze kukamilisha ujenzi huo, na ifikapo mwezi wa tatu Mwishoni ujenzi huo uwe umekamilika na wanafunzi wapate madarasa yao waendelee kuyatumia.

" niwatake Wahandisi wa halmashauri kwa kushirikiana na Watendaji wa kijiji kuwasimamia mafundi kwa karibu ilikuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati endapo mtashindwa kusimamia ipasavyo tutawajibishana, Wananchi wamejitahidi kuchangia na Serikali imetoa fedha kwa wakati ni lazima muhakikishe mnakamilisha suala hili ilikuwatia moyo wananchi kuendelea kuchangia jitihada za Serikali",alisema Kanali Ndagala.

Hata hivyo Ndagala alisema katika Wilaya hiyo kuna upungufu wa madarasa ambapo mpaka sasa juhudi za kumaliza changamoto hiyo inaendelea kwa kuhakikisha Wananchi wanachangia kwa kushirikiana kujenga na kufyatua tofari na serikali inasaidi a kiasi kidogo cha fedha pamoja na kuezeka bati katika majengo hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kakonko, Novatus kalobagwa alisema Shule hiyo ina zaidi ya Wanafunzi 1000 na ina madarasa tisa ambapo matano yamekamilika na manne yanaendelea kujengwa , hali hiyo inapelekea kila darasa kuwa na Wanafunzi 100-105 hali inayo pelekea mwalimu kuwa na wakati mgumu katika ufundishaji.

Alisema kutokana na Changamoto hiyo bado Wanafunzi katika shule hiyo wanaendelea kufauru, ambapo mwaka jana Wanafunzi wote wa darasa la saba Walifauru kwa asilimia miamoja na watano walipelekwa katika shule za vipaji maalumu kutokana na ufauru wao kuwa mzuri.

Aidha aliiomba serikali kihakikisha inamaliza kero hiyo kutokana na Maelekezo ya elimu ni kwamba ilikuhakikisha Mwanafunzi anaelewa ni lazima darasa moja liwe na Wanafunzi 45 kila chumba ambapo itamsaidia mwalimu kujua maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja na kuongeza ufauru kwa kiasi kikubwa.
 Sehemu ya Madarasa hayo ambayo bado hayajakamilika
 MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Kakonko,alipofana ziara ya kukagua madarasa manne na ofisi mbili zilizoko katika ujenzi katika shule hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akikagua ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili katika Shule ya Msingi Kakonko Wilayani humo, ambapo alibaini kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi kwa mafundi hali iliyo pelekea kusua sua kukamilika kwa ujenzi huo.

No comments:

Post a Comment