Friday, March 10, 2017

WAKURUGENZI WA SHIRIKA MISAADA YA KIMAENDELEO LA UINGEREZA WAWATEMBELEA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WILAYANI KISARAWE,MKOANI PWANI.



Mkurugenzi Mtendaji waShirika la Misaada ya Maendeleo la Uingereza DFID katika Benki ya Dunia Bw.David Kinder amepongeza hatua iliyofikiwa na serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- katika kuteleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini,PSSN.

Bw. Kinder ametoa pongezi hizo baada ya kukutana na walengwa wa Mpango huo katika vijiji vya Mzenga A na Vilabwa katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambako amejionea mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta za uboreshwaji wa makazi,elimu,lishe na afya kwa walengwa hao.

Amesema hatua iliyofikiwa na walengwa hao inapaswa kuungwa mkono zaidi ili hatimaye waweze kuondokana na madhira ya umasikini unaowakabili.

Kwa upande wao, baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika vijiji hivyo wamesema tangu kuanza utekelezaji wa Mpango huo wameanza kuona fursa za maendeleo ikiwemo kuezeka mabati nyumba zao, kufuga kuku, na hata kuongeza shughuli za kilimo.

‘’Sikuwahi kuota kuwa siku moja nitamiliki na kuishi kwenye nyumba ya bati,lakini kupitia TASAF nimeweza , ninaishukuru sana serikali na TASAF kwa mpango huu mzuri’’ alisisitiza bi. Asha Khalifan Kikombe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 hivi.

Amesema ili kufikia mafanikio hayo amekuwa akinunua mabati kidogo kidogo kila anapolipwa ruzuku hiyo na hatimaye kumwezesha kupata mabati yaliyotosheleza kuezeka nyumba yake na kuondokana na adha ya kuishi katika nyumba iliyoezekwa kwa majani.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kisarawe B. Happinness William Seneda ameshukuru nchi wahisani wa mpango wa kunusuru kaya masikini kwa kuiunga mkono serikali ya Tanzania katika jitihada za kuwaondolea kero ya umasikini wananchi wake.

Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika vijiji vya Vilabwa na Mzenga A pia hutekeleza mpango wa ajira ya muda kwa miradi wanayoibua wakati wa kipindi cha hari (kigumu) ukiwemo ukame,mafuriko na kisha kulipwa ujira ikiwa ni sehemu ya kuwaongezea kipato.


Bi.Asha Khalifan Kikombe mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotelezwa na TASAF katika kijiji cha Vilabwa ,Wilaya ya Kisarawe ,mkoani Pwani akiwaonyesha wageni kutoka Shirika la Misaada la  Uingereza (hawako pichani) nyumba aliyoezeka kwa mabati alizozinunua kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF
Ujumbe kutoka DFID wakiwa na baadhi ya watendaji kutoka TASAF na Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe wakipata maelezo ya mradi wa kutunza  mazingira unaotekelezwa na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini kwa utaratibu wa Ajira ya Muda unaotekelezwa wakati wa kipindi cha hari kwa lengo la kuwaongezea walengwa kipato.
Baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Msikini katika kijiji cha  Mzenga A wilaya ya Kisarawe wakishiriki katika mkutano ulioitishwa kuzungumzia mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Mpango uliohudhuriwa pia na wageni kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID.
Ujumbe kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID ukipata maelezo kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Vilabwa juu ya namna alivyonufaika na fedha zinazotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jmii TASAF.

Bi.Asha Khalifan Kikombe mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotelezwa na TASAF katika kijiji cha Vilabwa ,Wilaya ya Kisarawe ,mkoani Pwani akiwaonyesha wageni kutoka Shirika la Misaada la Uingereza (hawako pichani) nyumba aliyoezeka kwa mabati alizozinunua kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF.
Ujumbe kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID ukipata maelezo kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Vilabwa juu ya namna alivyonufaika na fedha zinazotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jmii TASAF.

No comments:

Post a Comment