Sunday, June 11, 2017

: Kamanda Wa Polisi Mara Amethibitisha Kuhusu Basi Lililoungua





Basi la kampuni ya Batco lililokuwa likitokea Sirari kuelekea Mwanza muda mfupi baada ya kuvuka Mto Mara lilianza kufuka Moshi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jaffari Mohamed akizungumzia tukio hilo amesema wanafuatilia kubaini chanzo cha ajili hiyo iliyosababisha mali za abiria kuteketea kwa moto, huku abiria 75 waliokuwamo wakinusurika kifo.
Basi hilo lilianza kuteketea moto leo (Jumamosi) saa saba mchana eneo la Kirumi, Kata ya Bukabwa wilayani Butiama.
Kamanda wa Polisi Mara Jafari Mohamed anazungumzia kuhusu ajali hiyo......

No comments:

Post a Comment