KATIKA
hali ya kushangaza na kusikitisha,mkazi wa moshi bar Manispaa ya
Ilala,amedaiwa kumuunguza wifi yake( 15) sehemu zake za siri na
kumsababishia maumivu makali.
Hayo yametokea jana Jijini Dar es
Salaam, baada ya askari polisi wa kituo cha Stakishari, kupokea taarifa
kutoka kwa majirani juu ya unyama huo aliofanyiwa binti huyo.
Polisi
hao mara baada ya kupata taarifa hiyo, walifika nyumbani kwa mtuhumiwa
lakini iliwachukua zaidi ya saa mbili kufanikiwa kumtoa ndani mtuhumiwa
ambaye alidaiwa kujifungia.
Hata hivyo, hali ilikuwa tete baada
ya wakazi na majirani wa eneo hilo walioguswa na tukio , walipoamua
kuvamia nyumba hiyo baada ya kupokea taarifa za uongo kuwa mtuhumiwa
hayupo na kuamua kuwashinikiza polisi wamtoe au wajichukulie sheria
mkononi.
Kufuatia mvutano huo, Polisi waliofika kumchukua
mtuhumiwa , walizidiwa na kuamua kuondoka kwa lengo la kwenda kuongeza
nguvu kwa kuongeza askari na mabomu ya kurusha ili kuweza kuwatanya
wananchi waliokuwa na hasira.
Licha ya kuongeza askari, haikuwa
kazi rahisi kuwatawanya mpaka walipoamua kupiga risasi hewani na
kufanikiwa kuwatawanya wakazi hao waliokuwa na hasira sambamba na kumtoa
mtuhumiwa aliyekuwa amejificha juu ya dari ya nyumba.
Mtoto
aliyefanyiwa unyama huo alisema, Mei 30, alilazimishwa kunywa maji
ambayo yamechanganywa na vipande vya glasi huku akiwa anapigwa na waya
wa umeme.
Alisema siku iliyofuata Mei 31, alipigwa na mama huyo
na baadaye kuingizwa kipande cha mti sehemu za haja kubwa ambacho
alikaa nacho kwa saa mbili na baadaye mama huyo alimtoa. “Nilikunywa
maji yaliyochanganywa na vipande vya chupa ya bilauli huku nikiwa
napigwa ambavyo vinaniletea matatizo ya tumbo ambapo nimepata choo siku
moja hadi leo hii sijapata tena ambacho kilikuwa na damu nyingi”alisema
Juni
1, mwaka huu majira ya saa 8 mchana mtoto huyo ndiyo alichomwa moto
katika sehemu zake za siri, huku akiwa amefungwa mikono na miguu kwenye
dirisha.
Alisema siku hiyo alianza kumpiga kwa saa moja na
baadaye alimkamata na kumfunga kamba kwenye miguu na mikono huku
akichukua moto na kumuunguza sehemu zake hizo za siri na kumsababishia
maumivu makali.
“Nilivuliwa nguo zote na alinifunga kamba huku
akichukua moto na kuniweka sehemu zangu zote za siri ambapo kwa sasa
nashindwa kwenda haja kubwa na ndogo.
Jirani Aziza Saidi alisema,
Juni 2, mwaka huu walimuona mtoto huyo akielekea dukani huku akiwa
amepanua miguu yake ndipo walipomwita na kumuuliza na aliwajibu kuwa
ameunguzwa na moto sehemu zake za mwili.
Alisema walimwita ma kumwangalia sehemu zake na kukuta zimeharibika ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa dada yake ili amchukue.
Mtuhumiwa
huyo katika utetezi wake alisema, hawezi kufanya vitendo kwa wifi yake
na anajua uchungu wa kuzaa kwa sababu yeye ni mama wa watoto wawili.
Mtoto huyo alipelekwa katika hospitali ya Amana kwa uchunguzi zaidi. |
No comments:
Post a Comment