Saturday, June 9, 2012

Maandamano ya Waislamu yapigwa marufuku

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesitisha maandamano yaliyoandaliwa na Shura ya Maimamu Tanzania leo kwa lengo la kulipinga Baraza  la Mitihani la Taifa (Necta) kuwafelisha wanafunzi wa Kiislamu wa kidato cha sita.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Ahmedi Msangi, alisema jana kuwa Jeshi hilo halioni sababu ya lufanyika kwa maandamano hayo na badala yake aliwataka wahusika kufanya mkutano pekee.


Msangi alisema sababu za kusisitisha maandamano hayo ni jeshi hilo kutoa ulinzi wa kutosha kwa kuwa waumini watakuwa wametoka katika katika misikiti mbalimbali baada ya ya sala ya Ijumaa.

“Itakuwa ni vigumu kwa Jeshi kujipanga ili kuimarisha ulinzi, ni vema wakaendelea na mkutano wao waliopanga kufanya kwenye viwanja vya  Kidongo Chekundu,” alisema.

Alisema kuwa kama wataruhusu maandamano hayo ikitokea vurugu utakuwa vigumu kwao kuthibiti. Msangi alisema yeyote atakayekaidi amri hiyo atakiona cha mtema kuni.
CHANZO: NIPASHE
 

No comments:

Post a Comment