Rais wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour
Baada ya kutinga hatua hiyo, Zanzibar Heroes sasa itajitupa uwanjani leo kupambana na timu ya taifa ya Cyprus katika mchezo utakaofanyika saa tatu na nusu usiku kwenye uwanja wa Suleimani ya nje ya Mji wa Erbil huko Kurdistan.
Taarifa kutoka Kurdistan zimeeleza kwamba Zanzibar Heroes imezua gumzo kubwa tangu kuanza kwa mashindano hayo Juni 4 mwaka huu hasa baada ya kutoa kipigo cha 6-0 dhidi ya Ratia katika mechi ya ufunguzi.
Mabao ya jana ya Zanzibar Heroes yalifungwa na Khamis Mcha 'Viali' katika dakika ya 22, Amir Hamad (dakika ya 61) na Awadh Juma (dakika ya 90).
Mechi nyingine ya nusu fainali itazikutanisha timu ya taifa ya Province iliyopo Ufaransa dhidi ya wenyeji Kurdistan, na fainali ya michuano hiyo itafanyika Juni 9 saa kumi za jioni katika uwanja wa Taifa wa Kurdistan.
Zanzibar kwa mara ya mwisho ilitwaa kombe la Chalenji mwaka 1995 nchini Uganda, ambapo aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour aliwazawadia pikipiki mpya aina ya Vespa kila mchezaji.
No comments:
Post a Comment