Monday, June 11, 2012

Mawakili wa ICC waliokwenda kuonana na Seiful Islam Gaddafi watiwa mbaroni nchini Libya


Seiful Islam
Seiful Islam Gaddafi, mwana wa kiongozi wa Libya aliyeuawa katika harakati za mapinduzi
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imesema kuwa, mawakili wanne wa mahakama hiyo walioelekea nchini Libya kwa ajili ya kuonana na Seiful Islam, mwana wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi aliyeuliwa katika wimbi la mapinduzi, wametiwa mbaroni na viongozi wa nchi hiyo.

Mkuu wa Mahakama ya ICC, Sang-Hyun SONG, raia wa Korea Kusini ameeleza kuwa ana wasiwasi na usalama wa mawakili hao na amewataka viongozi wa Libya wawachilie huru mara moja.
SONG pia amesema, wana wasiwasi sana na hali ya mawakili hao hasa kwa vile hakuna mawasiliano yoyote yaliyopo baina yao na mawakili hao.
Taarifa zinasema kuwa, mmoja wa mawikili hao walikuwa na nia ya kusimamia upande wa kutetea haki za Seiful Islamu Gaddafi. Hata hivyo amefungiwa nyumbani katika mji wa Zintan kutokana na kuthibitika kuwa alitaka kumpelekea nyaraka za siri na za hatari, Seiful Islam.
Viongozi wa hivi sasa wa Libya wanataka mwana huyo wa Kanali Muammar Gaddafi ahukumiwe nchini humo na kwa sheria za Libya wakidai kuwa tuhuma zinazomkabili ni za makosa aliyoyafanya ndani ya nchi hiyo.
Hata hivyo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, inang'ang'ania ahukumiwe na mahakama hiyo nje ya Libya.

No comments:

Post a Comment