Mwinjilisti Reinhard Bonnke.
Amani kwa miaka mingi ,imekuwa ni tunu
maalum kwa taifa hili,kwa kutambua umuhimu wa amani kwa watanzania,Muungano wa
makanisa ya kipentekoste Tanzania ndani ya Jiji la Dar es salaam,wameamua
kuenzi amani kwa kupitia mkutano wa Injili utakaokuwa na kauli mbiu''utii wa
sheria bila shuruti''
akifungua rasmi maandalizi ya mkutano wa
injili wa siku zipatazo 5 ,kuanzia tarehe 21 mwezi wa nane hadi tarehe 25 mwezi
wa nane mwaka huu,makamu mwenyekiti wa
mkutano huo wa maandalizi ya
mkutano wa Amani askofu Dkt Bruno wa kanisa la kipentekoste amesema ,makanisa yote yakipentekoste
yameungana na serikali kwa kupitia jeshi la polisi Tanzania katika suala zima
la kuhibiri amani kwa kutii sheria bila
shuruti.
Katika ufunguzi huo askofu Dr. Bruno
ameishukuru serikali pamoja na mkuu wa polisi IGP Saidi Mwema,kwa kuwapa kibali
kwa njia ya waraka cha kuhubiri
amani,utii bila shuruti katika mkutano wa wazi
wa kuhubiri amani utakaoanza
tarehe 21 mpaka 25 mwezi wa nane katika
uwanja wa jeshi la wokovu nyuma ya
uwanja wa Taifa .
hili ndilo kanisa la mwinjilisti Reinhard Bonnke |
Katika mkutano huo mwinjilisti wa kimataifa
kutoka marekani katika kanisa la kipentekoste la ALL CHRIST NATION Mhubiri
REINHARD BONNKE.
REINHARD BONNKE ni mwinjilisti mwenye sifa
kubwa ya kufanya mahubiri na kuzunguka
dunia nzima akihubiri na kutangaza neno la Mungu na kwa Tanzania alipata
kuhubiri katika viwanja vya shule ya secondari karibu na viwanja vya Nmc na
takribani watu 145,000 walihudhuria mkutano huo wa mwinjilisti wa kimataifa
na mtumishi wa Mungu Reinhard Bonnke.
Mkutano huo utakuwa ukianza saa 9 alasiri
na kumalizika saa moja kamili usiku.
Jeshi la polisi limeridhia kufanyika kwa
mkutano huo nao wamehaidi kutoa ulinzi wa kutosha kwa wananchi watakaohudhuria
mkutano huo wa kudumisha amani,kutii sheria bila shuruti.
Nae akielezea mkutano huo katibu wa mkuu wa
Dr. Askofu David Mwasota amewaalika viongozi wa vyama vya siasa kuhudhuria
katika mkutano wa kutii sheria bila shuruti ,kwani ni wakati wao wa kufika
kupata baraka za Mungu nao ka,a wanasiasa
kwenda kuhubiri sheria ya utii bila shuruti kwa wafuasi wao.
Benin. CfaN Gospel Crusade, Nov. 2012.
Wakati huo huo Dr.David Mwasota ametoa
shuhuda za kusisimua jinsi majambazi walivyotii sheria bila shuruti kwa
kujisalimisha kanisani na kuachana na
vitendo vyote vya ujambazi kwa kutii sheria bila shuruti.
Akiendelea kitoa shuhuda amesema dada mmoja
katika mkutano wa injili ,alijiweka wazi kwa
kujitangaza kuwa alikuwa na tabia ya umalaya ,kwani alokuwa na tatizo la
kupenda kila mwanaume anayepita mbele yake na alikuwa na mbinu za kipekee pindi
apendapo mwanaume,na hakuna mwanaume ambaye yeye alimpenda na akamkosa lakini
alitii sheria bila shuruti na kuamua kuachana na umalaya na alipouliza na
Mwinjilisti Dr .David Mwasota kama anampenda afande aliyekuwa katika mkutano
huo, binti huyo alisema kwa sasa haoni mwaume yeye na kusema kwa sasa nini yeye
na yesu peke yake.
huu ni mkutano ulifanyika huko Abidjan, Côte d'Ivoire. na watu 85,000 walihudhuria kwa siku ya kwanza
Nae Mchungaji Bathelomeo Shega ambaye ni
mwenyekiti wa uhamasishaji katika
mkutano huo amezidi kuimwagia sifs serikali na jeshi la Polisi kwa kuwapa
waraka wa kuwawezesha kuhubiri amani kwa kutumia kauli mbiu ya utii wa sheria
bila shuruti.
huu ni mkutano ambao mwinjilist Reinhard Bonnke alihuburi huko sydeny
Nae mchungaji Absalom Mwalubalile amesema
zaid ya kwaya 5000 zitaimba ktika mkutano huo ndani yake kukiwa na waimbaji
mbali mbali maarufu wa nyimbo za injili pamoja na wahudumu wapatao elfu 50.
No comments:
Post a Comment