Thursday, July 11, 2013

Jeshi Polisi latakiwa kuwachukulia hatua wabakaji wa watoto



Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar 

Na Ali Issa  Maelezo  Zanzibar
IMEELEZWA kuwa Jeshi la Polisi na Mahakama bado hawajalichukulia hatua za makusudi suala la ubakaji watoto ambalo  linaonekana likiendelea kuongezeka siku hadi siku.  
Kutolichukulia hatua  huko ni pamoja na adhabu ndogo wanazo pewa wahalifu  na kutoridhishwa na ushahidi wa kuona unao tolewa na watu mbali mbali mahakamani.

Hayo yamesemwa leo huko katika ukumbi wa  Baraza la wawakilishi  chukwani   wakati walipokuwa wakichangia bajeti ya Wizara ya Ustawi wa Jamii ,Vijana Maendeleo ya Wanawake na Watoto juu  ya suala zima la udhalilishaji na ubakaji  wa watoto  ulivyokithiri hapa nchini.

Wamesema hali hiyo mbaya  inatokana na jeshi   hilo na Mahakama kutochukua  hatua za makusudi za kisheria kwa watuhumiwa ambao wanahusika na kesi za uzalilishaji watoto na  na kuwachilia kuwapa adhabu ndogo au kuto kamilika ushahidi wakuona.

“Polisi wanataka ushahidi  wa aina gani ? kila siku suala la ubakaji linaongezeka hivi karibuni mtu kafungwa miezi sita kwa kosa la ubakaji hio ni adhabu ndogo  kulingano na kosa lenyewe, alisema mmoja wawalikilishi hao.
Aidha walisema kuwa masuala ya udhalilishaji yanafanywa na watu wazima wenye akili zao timamu jambo ambalo linawasababisha   watoto hao kuona aibu  na kuweza kuathirika kisaikolojia.

Naye Farida Amour Mohamed, alimuomba Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kulishughulikia suala hilo kwa  makini ili uzorotaji wa kesi pamoja na hukumu  zisicheleweshwe.

Naye Asha Bakari Makame mwakilishi wa viti maaluma wanawake  amesema suala la ubakaji watoto linauma sana hasa kwa sisi wazazi ,kwahivyo kama kuna tatizo la kisheria lirekebishwe haraka sana.
“Hatuta kubali kabisa kabisa  Taifa la kesho kudhalilishwa, Wizara hii ndio iliyozaa marais,i mawaziri, duniani   kote  hii ni wizara nyeti “alisema Asha Bakari.

Mwakilishi huyo aliiomba  Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar  kutoa  nafasi maalum  ya msaada kwa   Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana wanawake na Watoto   kutopewa  nafasi  mtuhumiwa  yeyote wa  ubakaji  wa watoto na hatua kali zichukuliwe  dhidi yake.

Aidha, wawakilishi hao walisema kuwa  kutokana na  sula hilo  la kutokamilika ushahidi  wa kesi za uzalilishaji ikiwa unaonekana kuwa haukidhi haja, serikali itafute kifaa maalumu cha kipimo  kinacho tumia utalamu DNA ili kuweza  kugundua ushahidi wa uhakika ili vyombo vya sheria viridhike.

Wakilishi hao kwa umoja wao walilani suala la omba omba ambalo linachukuwa nafasi kubwa hapa nchini pamoja kutumishwa kazi watoto wakiwa na umri mdogo.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya alijibu suali la  nyongeza la muakilishi viti maalumu  Panya Ali Abdalla aliyetaka kujua  kwanini serikali na washirika wa maendeleo watumia pesa  nyingi kujenga  nyumba  za Daktari katika vituo vya afya  na kwa nini nyumba hizo hadi sasa hazikaliwi na madaktari ?

Alisema kuwa ni kweli  kuna baadhi ya vituo vya afya vimejengewa nyumba za  kukaa madaktari kama vile ukongorani na  sehemu za Pemba, nyumba hizo zimepelekewa  Madaktari kuzikaa  lakini kwa makusudi madaktari waliopelekwa nyumba hizo hawataki kuzikaa kwa madai waume zao hawataki  na wengine wamejitia sababu za kutaka  kuimarisha maisha yao.

Alisema watu hao iwapo hawatakua na sababu za kimsingi kuna hatari kufutiwa posho ambazo zime ambatanishwa na ishahara yao kwa kukiuka agizom la wizara kuukaa katika vituo hivyo.

Aidha alisema kwa wale abao nyumba haziko na hawajakataa kukaa karibu na vituo nap engine wanatumia nauli zaidi maramoja kweli hao inafaa wafikiriwe na watachukua hatua kulifanyia kazi vipi waone kuwasaidia.  

habari kwa hisani ya bayana blog

No comments:

Post a Comment