Thursday, July 11, 2013

WANAHABARI WAASWA KUEPUKA KUANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI KATIKA KONGAMANO LA AMANI


Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Centre for Democracy (TCD), ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia akimkabidhi Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete maazimio ya Kongamano la Kitaifa la kujadili Amani ya Taifa, lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam na kufungwa leo jioni.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la Kitaifa la Kujadili Amani ya Taifa, lililofanyika katika hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salam leo jioni.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la Kitaifa la Kujadili Amani ya Taifa, lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salam leo jioni.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki katika Kongamano  la Kitaifa la Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Kushoto ni kiongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia (MB), Mwenyekiti wa TLP, Augustine Lyatonga Mrema (watatu kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Momose Cheyo.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Vyama vya Siasa na washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Freddy Maro)

Na Claudia Kayombo
RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa hali ya amani nchini si shwari na kwamba iwapo hazitachukuliwa hatua madhubuti za kuondoa kasoro ndogondogo amani ya nchi itafika pabaya.

Pia ameonya kuwa  iwapo kila chama nchini kitaanzisha jeshi la mgambo kwa ajili ya kupigana kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
 
 Rais Kikwete aliyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga kongamano la siku mbili la kutafakari amani ya Taifa lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania lililowashirikisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa na Serikali.

Alikiri kuwepo viashiria dhahiri vya uvunjivu wa amani kwa kuwa kuna watu wakiwapiga wenzao,kuwaumiza na kuwaua na kutaka jitihada za haraka zinahitajika kabla mambo hayajaharibika.

Alisema hali kwa sasa siyo nzuri kwa upande wa amani ya nchi na ni jukumu la kila mmoja kuhimiza amani kwa kuwa amani ikishapotea hata serikali itashindwa kufanya kazi za kuwaletea maendeleo wananchi nao na wananchi watashindwa kufanya shughuli zao za uzalishaji mali kwa kuwa risasi zitakuwa zinarindima kila upande.
 
Kauli hiyo ya rais Kikwete imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kutangaza azma yao ya kuanzisha kukundi cha kujilinda kwa madai kuwa vyombo vya dola vimeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juzi.
 
Alisema chama hicho kutokushiriki katika kongamani hilo la amani siyo maamuzi sahihi lakini alikipongeza kwa kuwa kilishiriki katika maandalizi ya kongamano zima lakini wakashindwa kushiriki katika kongamano.
 
Alisema katika viashiria vya uvunjivu wa amani kuna vyama vya siasa na viongozi wa dini wanachochea hivyo watu kama hao wanatakiwa kuonywa kupitia makongamano kama hayo.
 
Akizungumzia vyombo vya habari alisema vyombo hivyo vinatakiwa kutumia uhuru wao kuendeleza amani badala ya kuje nga na mwandishi wa habari akiandika habari ya uchochezi na kusababisha madhara atahukumiwa huku akitolea mfano mauaji yaliyofanyika nchni Rwanda yalisababishwa na uchochezi wa vyombo vya habari.
 
Aliongeza kuwa kituo cha demokrasia nchini kuandaa kongamano litakalowashirikisha waandishi wa habari kwa kuwa ni wadau wakubwa katika kuhamasisha amani.
 
Awali Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini akizungumzia maazimio ya kongamano hilo ni kuwepo  kuboresha mfumo wa kudumisha amani,kuanzisha kituo cha amani,kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo kabla ya umwagikaji damu,
Maazimio mengine ni kituo hicho kiwe na ubia na jeshi la polisi kupitia mafunzo kwa wanasiasa,sheria ya uanzishwaji wa vyama vya siasa ifanyiwe mabadiliko,wanasiasa waache kutumia lugha za matusi kudhalilisha mamlaka zilizopo madarakani.

No comments:

Post a Comment