Wednesday, January 8, 2014

Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akifungua kikao cha Bodi jijini .

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mwendahasara Maganga, akichangia wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam . (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, wakisikiliza michango iliyokuwa ikiwasilishwa na wajumbe wa bodi hiyo katika kikao chake hicho jijini Dar es Salaam .
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, akichangia mada wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara baada ya kufunguliwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki jijini .

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtevu akichangia wakati wa kikao hicho cha Bodi ya Barabara ya Mkoa.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, akichangia katika kikao hicho cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, Dar es Salaam .
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, akichangia katika kikao hicho cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akifafanua jambo, wakati akikiongoza kikao hicho, mara baada ya kukifungua leo asubuhi jijini Dar es Salaan. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan na kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando. 
Mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo, kutoka Sumatra, akichangia mada katika kikao cha bodi hiyo, jana jijini.
Mbune wa Kawe, Halima Mdee, akichangia kwenye kikao hico cha Bodi ya Barabara jijini .
Mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo, akichangia mada katika kikao hicho, jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akifafanua jambo, wakati akikiongoza kikao hicho, mara baada ya kukifungua leo asubuhi jijini Dar es Salaan. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan na kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akikikiendesha kikao cha Bodi ya Barabara, mara baada ya kukifungua leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mbunge wa ,Kinondoni, Idd Azzan na kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akifafanua jambo, wakati akikiongoza kikao hicho, mara baada ya kukifungua leo asubuhi jijini Dar es Salaan. Kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akifafanua jambo, wakati akikiongoza kikao hicho, mara baada ya kukifungua jana asubuhi jijini Dar es Salaan. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan na kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akifafanua jambo, wakati akikiongoza kikao hicho, mara baada ya kukifungua jana asubuhi jijini Dar es Salaan. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan na kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando.



Wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakimsikiza Mwenyekiti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Sadiki, wakati alipokuwa akifafanua jambo.




HOTUBA YA UFUNGUZI WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA YA MKOA WA DAR ES SALAAM TAREHE 07/01/2014

 

Mhe. Idi Azzan (Mb)   -     Makamu Mwenyekiti wa Bodi

                                      ya Barabara, Mkoa wa

                                      Dar es Salaam

 

Ndg. Theresia Mmbando – Katibu wa Bodi ya Barabara          

                                      Mkoa

 

Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya,

Waheshimiwa Wabunge

Waheshimiwa Wastahiki Mameya,

Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali zote za Mitaa, Mkoani kwetu,

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ‘DART Agency’,

Wajumbe wa Bodi ya Barabara,

Waalikwa, Mabibi na Mabwana.

 

Itifaki imezingatiwa.

 

Asalaam Aleikum,

Awali ya yote tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuumaliza mwaka 2013 kwa salama na kutujalia kuingia mwaka 2014 kwa salama. Niwatakie nyote mliohudhuria kikao hiki heri na fanaka katika mwaka mpya wa 2014.

 

Naomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha katika kikao hiki cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wetu.  Hiki ni kikao cha kwanza cha Bodi hii katika mwaka huu wa fedha (2013/2014).

 

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwenu nyote kwa ushirikiano mnaoendelea kutoa katika kusimamia maendeleo katika Mkoa wetu wa Dar es Salaam.  Mafanikio tunayopata yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano wenu katika kufuatilia ujenzi wa miundombinu ya barabara za Mkoa wa Dar es Salaam.  Naomba tuendelee na ushirikiano huo ili tuendeleze Mkoa wetu kioo cha maendeleo ya nchi yetu.

 

Ndugu Wajumbe,

Agenda kuu ya kikao hiki ni kupata taarifa za utekelezaji wa mipango na bajeti ya matengenezo ya barabara ya robo kwa kwanza ya mwaka huu wa fedha 2013/2014.

 

Tunaishukuru Serikali kwa kututengea katika Bajeti ya mwaka huu wa (2013/2014) fedha za barabara kwa Mkoa wa Dar es Salaam jumla ya shilingi 79,411,306,680.00. Kiasi hiki ni pamoja na fedha zilizotolewa kwa Meneja wa TANROADS Mkoa pamoja na Halmashauri zote kwa mchanganuo ufuatao:-

 

 

1. Kutoka kwenye Mfuko wa Barabara (Roads

    Funds).

         TANROADS      - Shs.    56,203,520,000/=     

         Ilala         - Shs.      1,964,380,000/=

         Kinondoni  -          5,528,410,000/=

         Temeke    -       1,313,880,000/=

   Jumla Tsh. – “  65,010,190,000/=

 

 

      2. Kutoka vyanzo vya Halmashauri (Own

          Source)

          Jiji la Dar es Salaam        -  Shs.     50,000,000/=

         Ilala                        -        2,517,240,000/=

         Kinondoni                 -       5,385,000,000/=

         Temeke                   -       3,043,241,680/=

         Jumla  Tsh.               -    10,995,481,680/=

 

3.         Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mfuko wa Maendeleo/Ruzuku.

           Jiji la Dar es Salaam   - Shs.    200,000,000/=

          Ilala                        -      1,678,500,000/=

          Kinondoni                -           300,000,000/=

         Temeke                   -        1,227,135,000/=

         Jumla  Tsh.               -        3,405,635,000/=

          Jumla Kuu                 Shs. 79,411,306,680/=

 

Hata hivyo kiasi hiki cha fedha ni kidogo kulingana na mahitaji ya Mkoa.  Pamoja na hayo kama fedha hizi zikitumika na kusimamiwa vizuri mafanikio yanaweza kuonekana.

 

  TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA

  MATENGENEO YA BARABARA KWA (JULAI –

  SEPTEMBA 2013).

Robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha ilianza

tarehe 1/7/2013 na kuishia tarehe 30/09/2013.  Hali halisi ya utekelezaji hadi robo ya kwanza inaisha Mamlaka za

Serikali za Mitaa na Wakala wa Barabara (TANROADS)

walikuwa kwenye mchakato wa manunuzi. Hivyo kazi nyingi zilizofanyika ni zile za miradi ya viporo (roll-over) vya mwaka uliotangulia wa 2012/13.

Kipindi hiki ni cha mvua hivyo pamoja na jitihada

tunazofanya za kufanyia matengenezo barabara, mashimo mapya nayo yanajitokeza katika barabara zote za changarawe na za lami.  Mashimo yote ni kero ila ukikutana na shimo katika lami linakuwa ni kero zaidi na hatari kwa mwenye gari na watumiaji wengine wote wanajitahidi kulikwepa shimo hilo. Hivyo basi, kipindi kama hiki cha mvua Wahandisi wajipange zaidi kutumia ‘cold mix’ kuziba mashimo kwani kwa taarifa niliyonayo ‘material’ hiyo haiathiriwi na maji hata wakati wa kuiweka.

Mkoa wetu umekuwa ukikumbwa na mafuriko kutokana na Jiografia iliyopo na shughuli zingine za kibinadamu, tujipange kuchukua hatua za kujihadhari na mafuriko ili tuwaepushe wananchi kukumbwa na mafuriko, kwa mfano wakazi wa Buguruni Kisiwani, hivi karibuni walikumbwa na mafuriko sababu moja wapo ni ujenzi holela na nyingine ni watu kujenga na kuzuia njia/mkondo wa maji. Tabia ya kuwaacha watu wanajenga kama hakuna taratibu na sheria, tufike mahali tuseme basi. Sheria za kudhibiti ujenzi katika mito na Bahari zipo lakini nashangaa kwa nini hazisimamiwi ipasavyo na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Nimepata taarifa ya kuanza ujenzi wa mfereji wa Bonde la Mpunga, hii ni hatua nzuri. Hivyo nawataka wanao usimamia mradi huo TANROADS, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni mshirikiane na Mkoa kuhakikisha mradi huo unafanyika kwa wakati na kwa ubora ya hali ya juu.  Bado tatizo la usimamizi dhaifu ni kubwa jambo linalopelekea Mkandarasi kutekeleza kwa kiwango cha ujenzi duni na hivyo miundombinu husika kuharibika hata kabla ya kipindi cha matazamio.

Ndugu Wajumbe,

Taifa letu lina mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa ’Big Results Now’ kifupi BRN. katika mkakati huu sekta za kipaumbele zina malengo waliyojiwekea, chonde nawaomba Wajumbe wa bodi hii  tuwe imara hakutakuwa na msalie mtume. Kazi lazima ifanyike,

Naamini ‘tukiamua tunaweza’, kwani mandhari ya Jiji letu wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hali ya Jiji ilibadilika kabisa, nawapongeza wote waliofanikisha ziara ile kubwa na kuipa sifa nchi yetu.  Hivyo basi msimamo uwe ni ule ule katika kuhakikisha malengo tuliyojiwekea katika BRN Kimkoa yanafikiwa kwa asilimia mia. Kila mtu atimize wajibu wake ipasavyo, tuache kufanya kazi kwa mazoea. Hili litafanikiwa tukiwa wabunifu zaidi, makini zaidi na kuongeza usimamizi katika kazi zetu za kila siku.

Aidha tupange mipango yetu tukizingatia namna tutakavyo ondokana na msongamano katika Jiji letu ambayo ni changamoto kubwa

Ndugu Wajumbe nawaomba mchangie kwa ukamilifu mawazo na ushauri juu ya uboreshaji wa matengenezo ya miundombinu ya barabara katika Jiji letu ili tuondokane na matatizo yaliyopo. Kabla ya kikao hiki tulipata wasaa wa kukagua kazi zilizofanyika na zinazoendelea kutekelezwa.  Kila kikundi kitapata wasaa wa kueleza yale waliyoyaona na kukosoa, kutoa ushauri kwa uwazi ili tuweze kupata uthamani wa fedha (value for money) katika kazi za barabara zinazofanyika.

Kwa hayo machache naomba kusema kwamba kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa kimefunguliwa rasmi.

                         ASANTENI   SANA

No comments:

Post a Comment