Saturday, February 1, 2014

Kinana awaletea neema waendesha bodaboda wa Mbeya


 Katibu Mkuuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa abebwa na waendesha bodaboda alipofanya nao mkutano leo kwenye Ukumbi wa Mtenda, Soweto, jijini Mbeya, ambapo alizungumzia mambo mbalimbali likiwemo la kuinua kipato chao cha maisha.
Waendesha bodaboda Mkoa wa Mbeya, wakwa wamembeba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya kufurahishwa na hotuba yake.
Waendesha bodaboda wakishangilia baada ya Kinana kuwakuna kwa hotuba nzuri iliyolenga kuwasaidia kuboresha  maisha yao.
Sehemu ya umati wa baadhi ya bodaboda walioshiriki kwenye mkutano huo.

Katibu Mkuu wa Waendesha bodaboda Mkoa wa Mbeya, Msumba Mdiga akisoma risala ambayo ilielezea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Nape akihutubia katika mkutano huo, ambapo alwaasa kuachana na vyama vya upinzani ambavyo daima vimekuwa vikiwatumia kwenye maandamano yenye vurugu lakini  haviwasadii kimaisha.
Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mbeya, Vicent Mwashoma, akihutubia katika mkutano huo.
Waendesha bodaboda wakishangilia hotuba nzuri ya Kinana.
Kinana akihutubia katika mkutano huo, ambapo aliahidi kuwapiga jeki katika mambo mbalimbali likiwemo la kujenga vituo vya kusubulia abiria pamoja na kuboresha ofisi yao na mikopo ya ya pikipiki.
Kinana akimtambulisha Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya, Inspekta Isaack Lema (kulia) kutoka Jeshi la Polisi.
Kinana akiondoka huku akisindikizwa na maofisa wa CCM pamoja na viongozi wa Bodaboda. Hayo yote ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM. Maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa mkoani Mbeya Jumapili Januari 2. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

No comments:

Post a Comment