Tuesday, February 11, 2014

MDAU KIZITO ASHINDA MILIONI 10 ZA 'CHAMPIONI MAHELA' AKIWA KWENYE DALADALA


BAADA ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye, mshindi wa milioni 10 amepatikana kupitia droo ya Shinda Mahela na Championi ambaye ni Kizito George Chuka.

Droo hiyo iliyochezeshwa mbele ya Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao kwenye Viwanja vya Mbagala- Zakhem jana Jumanne.

Akizungumza Kizito ambaye ni makazi wa Kawe jijini Dar alipopigiwa simu na muendeshaji wa shughuli hiyo MC Chaku, mshindi huyo alikuwa ndani ya daladala hivyo hakuwa na mengi ya kuongeza zaidi ya kushukuru kwa kujinyakulia kitita hicho.

Kizito, 43 alionekana kufurahia kutokana na sauti yake kusikika akichekelea na haijafahamika kama aliwasilimulia abiria wenzake aliokuwa nao ndani ya daladala hiyo.

Hata hivyo keshokutwa Alhamisi anatakiwa kuja Ofisi za Global Publishers kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuchukua mkwanja wake huo.

“Nimefurahi sana lakini sasa hivi nipo ndani ya daladala naomba muda nikifika nitakupigia,” alisema Kizito.
Washindi wengine ambao walipatikana siku hiyo ni Athuman Yusuph, 40, mkazi wa Mwanza aliyejinyakulia shuka za kisasa na Amiri Kinguaba, 60 aliondoka na simu kali aina ya Samsung Galaxy.
MC Chaku (kushoto) akiwa na mmoja ya wakazi wa Mbagala tayari kwa kuchagua mshindi wa Championi Shinda Mahela.
...Kuponi za Championi Shinda Mahela zikiwa tayari kwa ajili ya droo.
Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao (kushoto), Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati) na kulia ni Ofisa Masoko wa Shinyanga Emporium, Herman Bernard wakiendelea kufuatilia droo.
...Mchezesha droo akichambua kuponi katika Viwanja vya Mbagaka Zakhem jijini Dar.
MC Chaku akimfunga kitambaa mkazi wa Mbagala ili amchague mshindi wa Championi Shinda Mahela
Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao (kushoto) akikabidhiwa kuponi ya mshindi wa milioni 10 za Championi Shinda Mahela.
MC Chaku (kulia) na mkazi wa Mbagala wakitaja jina la mshindi wa milioni 10 za shindano la Championi Shinda Mahela ambaye ni Kizito George.
MC Chaku akimwaga kuponi za Championi Shinda Mahela wakati wa mchakato wa kumpata mshindi wa milioni 10.
...MC Chaku akiweka sawa kuponi hizo.
Msomaji wa Championi kutoka Mbagala akitafuta mshindi wa tisheti.
Mr Championi (kushoto) akimkabidhi mshindi tisheti.
...Wakazi wa Mbagala wakiendelea kufuatilia Bahati Nasibu ya shindano la Championi Shinda Mahela.
Wasomaji wakijaza kuponi za Championi Shinda Mahela kabla ya Bahati Nasibu kuanza.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akiongea na wanahabari baada ya kupatikana mshindi wa Championi Shinda Mahela ambaye ni Kizito George.
Burudani wakati wa droo hiyo ya mwisho.
Burudani ikiwa imepamba moto Viwanja vya Mbagala Zakhem kabla ya droo ya mwisho ya kumpata mshindi wa milioni 10 kupatikana.

(PICHA/HABARI: DENIS MTIMA NA LUCY MGINA/GPL)

No comments:

Post a Comment