Saturday, May 10, 2014

Makamu wa Rais Dk. Bilal ayafunga maadhimisho ya Wiki ya Elimu mjini Dodoma leo


Makamu wa Rais Dkt Ghalib Bilal akimpatia cheti Mwanafunzi Nelson Athon wa shule ya sekondari ya 
Kizilego iliyopo mkoani Bukoba baada ya kufanya vizuri mwaka mjini Dodoma leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Ghalib Bilal akiwa na moja ya tuzo zilizotolewa kwa walimu wa Shule zilizofanya vizuri katika Elimu 2013 wakati wa kilele cha wiki ya Elimu leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi.
Wanafunzi na walimu ambao shule zao zimefanya vizuri wakiwa katika jukwaa maalumu walipokuwa wakisubiri tuzo na zawadi mbalimbali zilizotolewa na Makamu wa Rais Dkt. Ghalib Bilal wakati wa kilele cha wiki ya Elimu iliyohitimishwa leo, Jumamos Mei 10, 2014, iliyofanyika kitaifa Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Msalato Dodoma, akiwa ameshika mfano wa hundi ya milion 3 zilizotolewa na Serekali kama motisha kwa shule hiyo kutokana na kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwa mwaka 2012/ 13, motisha hiyo imetolewa kwa jumla ya shule 14 za sekondari na 46 za msingi nchini, wakati kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu.
Mshairi wa sanaa ya lugha katika muziki Mrisho Mpoto na Banana Zoro wakitoa burudani katika kilele cha wiki ya Elimu iliyofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma leo.
 Mshairi wa sanaa ya lugha katika muziki Mrisho Mpoto na Banana Zoro wakitoa burudani katika kilele cha wiki ya Elimu iliyofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma leo
Wanafumnzi Shule za Msingi na Sekondari wakiwa majukwaani na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki yaElimu yaliyofanyika mjini Dodoma leo.
 Wanafumnzi Shule za Msingi na Sekondari wakiwa majukwaani na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki yaElimu yaliyofanyika mjini Dodoma leo.
Wanafunzi wa Shule mbambali za Msingi na Sekondari wakiwa wamezagaa kutembelea mabanda ya maonyesho ya wadau wa Elimu katika siku ya mwisho ya maadhimisho ya wiki ya Elimu kabla ya kufungwa
Wanafunzi wa Shule mbambali za Msingi na Sekondari wakiwa wamezagaa kutembelea mabanda ya maonyesho ya wadau wa Elimu katika siku ya mwisho ya maadhimisho ya wiki ya Elimu  kabla ya kufungwa. (Picha zote na John Banda)

No comments:

Post a Comment