Monday, June 12, 2017

MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA MOTO ILIYOUNGUZA NYUMBA WILAYANI NYAMAGANA.

msangii-1
TAREHE 10.06.2017 MAJIRA YA SAA 18:30HRS KATIKA MTAA WA LUMUMBA KATA NA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MADUHU MASUNGA LIGUSHI @ MZEE SHINYANGA, MIAKA 75, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MTAA WA LUMUMBA, AMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ULIOUNGUZA NYUMBA YAKE KISHA KUJERUHI WATOTO WAKE WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.NGALULA MADUHU MIAKA 39, MFANYA BIASHARA NA MKAZI WA MTAA WA LUMUMBA, 2.BRIAN MADUHU MIAKA 26, MKAZI WA MTAA WA LUMUMBA, NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI NA VITU VILIVYOMO NDANI YA NYUMBA HIYO IKIWEMO KIASI KIKUBWA CHA FEDHA AMBAZO HADI SASA THAMANI YAKE BADO HAIJAFAHAMIKA.
INASEMEKANA KUWA KABLA YA AJALI HIYO YA MOTO KUTOKEA MAREHEMU ALIKUA NDANI YA NYUMBA YAKE YEYE PAMOJA NA WATOTO WAKE, NDIPO GHAFLA MAJIRA TAJWA HAPO JUU ULIZUKA MOTO MKALI ULIOKUWA UNAUNGUZA NYUMBA YAKE. INADAIWA KUWA KUTOKANA NA HALI HIYO MAREHEMU ALIKUWA AKICHUKUA BAADHI YA MALI ZAKE NDANI ILI AWEZE KUTOKA NAZO NJE NDIPO KWA BAHATI MBAYA MOTO ULIZIDI NA YEYE KUSHINDWA KUTOKA NJE NA KUPELEKEA KUUNGUA HUMO NDANI NA BAADAE KUFARIKI DUNIA NA MALI ZAKE KUTEKETEA.
AIDHA MOTO HUO ULIWEZA KUTHIBITIWA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA  POLISI, JESHI LA ZIMA MOTO NA UWOKOAJI PAMOJA NA TANESCO NA KUEPUSHA KULETA MADHARA MAKUBWA KWA BAADHI YA MAJENGO MENGINE YA BIASHARA YALIYOPO ENEO HILO.  AIDHA MOTO HUO UNGEWEZA KUDHIBITI MAPEMA LAKINI KUTOKANA NA MIUNDO MBINU YA ENEO HILO KUWA MIBOVU ILISHINDIKANA KWANI KULIKUWA NA UKUTA MKUBWA NA KUPELEKEA MAGARI YA MAJI YA JESHI LA ZIMA MOTO NA JESHI LA POLISI KUSHINDWA KUINGIA NA KUPELEKEA KUTOKEA KWA VIFO NA UHARIBIFU WA MALI.
THAMANI YA MALI NA VITU VILIVYOTEKETEA KATIKA AJALI HIYO YA MOTO BADO HAIJAFAHAMIKA, JESHI LA POLISI PAMOJA NA JESHI LA ZIMA MOTO KWA KUSHIRIKIANA NA TANESCO WANAENDELEA KUFANYA UCHUNGUZI NA UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO ILI KUJUA CHANZO CHA MOTO HUO, MAJERUHI WAMEPELEKWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KWA AJILI YA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA POLE KWA WANAFAMILIA WA MAREHEMU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWA MSIBA MZITO AMBAO UMEWAPATA MUNGU AWATIE NGUVU NA UVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU AMBACHO WANAPITIA, LAKINI PIA ANAWAOMBEA MAJERUHI WAPONE HARAKA ILI WAWEZE KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA AWALI, AIDHA PIA ANAWAOMBA WANAFAMILIA KUWA WAVUMILIVU WAKATI HUU AMBAPO POLISI WANAENDELEA NA UCHUNGUZI ILI KUWEZA KUFAHAMIKA CHANZO CHA AJALI HIYO YA MOTO. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUWEKA MIUNDOMBINU MIZURI/RAFIKI KWENYE MAKAZI YAO ITAKAYORUHUSU UOKOAJI WA VITU NA MALI PINDI ZINAPOTOKEA AJALI ZA AINA KAMA HII.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments:

Post a Comment